Dhamira ya dhati ya Marekani na ubia wake usioyumba na Tanzania

Dhamira ya dhati ya Marekani na ubia wake usioyumba na Tanzania

Kwa mara ya kwanza nilitembelea Tanzania zaidi ya miaka 30 iliyopita nilipofanya kazi kama daktari wa kujitolea katika hospitali ya umma huko Zanzibar. Katika kipindi hicho cha majira ya kiangazi ninachokikumbuka sana, niliwatibu watoto waliokuwa wakiugua utapiamlo, malaria, minyoo na kifua kikuu. Lakini pia nilivutiwa mno na watu wa Tanzania; walikuwa wema, wakarimu na wakiwachukulia …

Balozi Mpya wa Marekani Donald J. Wright awasilisha hati za utambulisho Ikulu leo kwa Rais John Magufuli

DAR ES SALAAM – Katika hafla iliyofanyika hivi leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dk. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho za Balozi Mpya wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Donald J. Wright. Dr. Wright anakuwa Balozi wa 19 wa Marekani nchini Tanzania. Balozi Wright alimhakikishia Rais Magufuli uimara wa …

Great Seal of the United States

Tamko kuhusu kushambuliwa kwa Freeman Mbowe

Ubalozi wa Marekani umestushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa Mbunge na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe hapo tarehe 9 Juni. Ubalozi unatoa wito wa kufanyika haraka kwa uchunguzi wa kina na huru na kisha kukamatwa na kushtakiwa kwa wale wote waliohusika katika shambulio hilo. Ubalozi unaliona tukio hili katili na …

Serikali Ya Marekani Kutoa Dola Milioni 2.4 Za Ziada Kusaidia Mapambano Dhidi Ya Janga La Covid-19

Dar es Salaam: Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 2.4 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5.6), ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya nchini Tanzania. Msaada huu unalenga kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara (laboratory capacity for optimal diagnostics), kusaidia jitihada …

Ushirikiano wa Marekani nchini Tanzania na duniani kote katika mapambano dhidi ya COVID -19

Dk. Inmi K. Patterson, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania  April 20, 2020 Simulizi za uongozi wa Marekani kwenye mapambano ya dunia dhidi ya Covid -19 ni simulizi za siku kadhaa, miezi na miongo. Kila siku msaada mpya wa kiufundi na vifaa unaotolewa na Marekani huwasili kwenye hospitali na maabara duniani kote. Jitihada …

Hatua Zilizochukuliwa na Serikali ya Marekani Kukabiliana na COVID-19 (3 Aprili, 2020)

Dar es Salaam: Serikali ya Marekani imejizatiti, na kila siku, kote duniani, inapiga hatua kukabiliana na changamoto ya kihistoria inayotokana na janga la COVID-19. Watu wa Marekani, kupitia taasisi za kiserikali, makampuni binafsi ya kibiashara, mashirika ya kiraia, mashirika ya misaada na vikundi vya kidini wametoa msaada mkubwa kwa waathiriwa wa virusi vya corona katika …

Toleo Jipya – Taarifa kuhusu covid19

Toleo Jipya: Machi 16, 2020 Miadi kwa ajili ya kupata viza zisozo za wahamiaji (Nonimmigrant visa) inaweza kufanyika kwa ajili ya safari za dharura kama inavyoelezwa katika kipengele kinachohusu maswali kuhusu miadi ya visa katika kiunganishi hapo chini. Aidha, kiunganishi hicho kinatoa maelezo ya jinsi ya kufanya uweze kupata miadi ya visa kwa haraka. https://ais.usvisa-info.com/en-tz/niv/information/faqs Kwa …

Taarifa Muhimu Kuhusu COVID19

Toleo Jipya: Machi 3, 2020 Raia wote wa kigeni ambao si wakazi halali wa kudumu wa Marekani na ambao walikuwa katika Jamhuri ya Watu wa China, isipokuwa katika mamlaka maalumu zinazojitegemea za Hong Kong and Macau, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au katika nchi zote za ukanda wa Schengen katika kipindi cha siku 14 kabla …