Flag

An official website of the United States government

Kamanda wa AFRICOM azuru Tanzania akiangazia ushirikiano katika nyanja ya usalama
4 MINUTE READ
Julai 28, 2021

Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku mbili nchini Tanzania, tarehe 27 na 28 Julai, ambapo alikutana na maafisa waandamizi wa jeshi na kufungua mazoezi ya kwanza ya pamoja ya kijeshi ya nchi hizi mbili toka mwaka 2017.

“Tanzania imeendelea kuwa nchi kiongozi barani Afrika katika nyanja ya usalama na mbia muhimu sana wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani.  Majeshi yetu ya ulinzi yana historia ndefu ya kufanya kazi bega kwa bega, na ziara hii ni kielelezo cha nia yetu ya kuimarisha zaidi ubia huo,” Alisema Jenerali Townsend.

Tarehe 28 Jenerali Townsend aliungana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika hafla ya ufunguzi ya mafunzo ya pamoja ya kijeshi (Joint Combined Exchange Training – JCET) kati ya askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na askari wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania katika Chuo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi. Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki sita ni ya kwanza ya aina yake kwa majeshi ya Tanzania na Marekani toka mwaka 2017.  Askari wa Kimarekani na wa Kitanzania watakuwa bega kwa bega wakishiriki mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao katika mbinu za medani kwa kikosi kidogo, ulengaji shabaha, utoaji matibabu, mbinu za kimapambano za kikosi kulingana na maeneo tofauti tofauti(unit maneuver), mafunzo kuhusu sheria za kivita au migogoro ya kivita (Law of Armed Conflict) na jinsi ya kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano.

“Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani inadhamira ya dhati kufanya kazi na Jeshi la Tanzania katika kutanzua changamoto za kikanda. Tunaimarisha ushirikiano baina ya majeshi yetu kupitia program mbalimbali za mafunzo na mazoezi ya pamoja,” alisema Jenerali Townsend. Aliongeza kuwa “Ni muhimu kukuza ushirikiano wetu na Tanzania ili kuendeleza malengo ya pamoja ya kiulinzi.”

Ziara Jenerali Townsend ilijumuisha pia kutembelea makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga, Jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua gwaride rasmi na kukutana na viongozi waandamizi wa jeshi hilo. Aidha, alitembelea Ubalozi wa Marekani alipokutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright na wafanyakazi wengine wa Ubalozi.

Kwa mujibu wa Balozi Wright, mazoezi haya ya kimafunzo na ziara ya Jenerali Townsend ni ishara ya umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano imara kati yake na Tanzania katika nyanja ya usalama.

“Ziara ya Jenerali Townsend inathibitisha ubia mpana na wa muda mrefu wa kiusalama kati ya Marekani na Tanzania. Tunaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano rasmi kati ya Marekani na Tanzania na ziara hii inasisitizia umuhimu wa ushirikiano wa kiusalama katika uhusiano huo uliojengwa katika kuheshimiana na maadili ya pamoja.