Childress Balozi akutana na Rais Magufuli

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress jana alifurahi kukutana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kujadili masuala mbalimbali kuhusu uhusiano rasmi na ubia imara baina ya nchi hizi mbili.  Balozi Childress na Rais Magufuli walijadili mipango ya kusainiwa kwa mkabata wa utoaji msaada kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID).  Chini ya mkataba huo ambao unaoanisha nafasi na wajibu wa nchi hizi mbili pamoja na Mpango – Mkakati wa miaka mitano wa USAID nchini (USAID’s five-year Country Development Cooperation Strategy, PDF 2.15 MB) USAID itaendelea kuwekeza zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 400 kwa mwaka katika miradi ya afya, kilimo, usimamizi wa maliasili, elimu, nishati na utawala bora nchini Tanzania. Programu hii ya USAID ni sehemu ya msaada wa jumla ya dola za Kimarekani milioni 800 unaotolewa kila mwaka na Marekani kwa miradi ya maendeleo na programu nyingine za ushirikiano zinazoendeshwa katika sekta mbalimbali hapa Tanzania kwa lengo la kuboresha afya, elimu, ukuaji mpana wa uchumi na kuimarisha usalama wa kikanda.