Arusha Yamkaribisha Kaimu Balozi Kwenye Ziara Ya Siku Mbili Yenye Shughuli Mbali Mbali

The CDA discusses the importance of community support for girls’ education in a press interview with ITV, during her site visit to Olkerian Primary School – beneficiary of an Ambassador’s Fund for HIV/AIDS Relief award.
Arusha Yamkaribisha Kaimu Balozi Kwenye Ziara Ya Siku Mbili Yenye Shughuli Mbali Mbali (Picha: Kwa Hisani Ya Ubalozi Wa Marekani)
Arusha Yamkaribisha Kaimu Balozi Kwenye Ziara Ya Siku Mbili Yenye Shughuli Mbali Mbali (Picha: Kwa Hisani Ya Ubalozi Wa Marekani)

Arusha, TANZANIA. Mnamo Novemba 15-16, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania na kwenye Jumuiya ya Afrika Masharika (EAC) Virginia Blaser alitembelea Arusha kwa shughuli mbali mbali na kukutana na watu na mashirika tofauti katika maeneo hayo. Ziara hiyo ilikuwa kielelezo cha ushirikiano imara na wa kudumu kati ya watu wa Tanzania na Marekani, na iligusia miradi ya pamoja inayokuza upatikanaji wa habari, mbinu bunifu za kilimo, ulinzi, afya na elimu bora, hususan kwa wasichana wadogo.     

Hapo Novemba 15, Kaimu Balozi Blaser alitembelea Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR), ambapo alikutana na Rais wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Jaji Sylvain Oré, pamoja na Makamu wa Rais na Msajili.  Baada ya mjadala kuhusu kazi za mahakama hiyo, Kaimu Balozi Blaser alitoa msaada wa vitabu tofauti vya sheria kwa maktaba kwa niaba ya Serikali ya Marekani. Baadae siku hiyo, alitembelea ECHO East Africa Impact Center, ambapo Mkurugenzi Erwin Kinsey, mfanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani Travis Silveus, na wenzao walielezea mbinu za kibunifu za kilimo, pamoja na uvumbuzi wa mbegu za mimea, kubeba maji na utayarishaji wa mahindi.  Kaimu Balozi Blaser alishuhudia kazi za kituo hicho alipotembelea shamba moja jirani, ambalo linatumia huduma za mafunzo za ECHO.  Siku ilikamilika kwa kutembelea Makumbusho na Kituo cha Utamaduni cha Arusha.

Kaimu Balozi Blaser aliianza siku ya Novemba 16 kwa kutoa somo la Kiingereza kwa wanafunzi 95 wa Shule ya Msingi Olkerian, ambapo shirika la Women and Child Vision (WOCHIVI) linajenga vyoo vya matundu kwa msaada wa $4,630 kutoka Mfuko wa Balozi wa Marekani wa kupambana na VVU/UKIMWI. Katika kukuza mazingira ya kiafya katika elimu, WOCHIVI watajenga vyoo sita shuleni hapo, ambapo sasa hivi kuna vyoo vinane kwa ajili ya wanafunzi na watumishi zaidi ya 800.  Wakati wa ziara yake, Kaimu Balozi Blaser alisisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia elimu, hususan kwa wasichana. “Kuhakikisha kwamba wasichana wanaendelea na shule siyo tu kwamba ni muhimu kwao ili kufikia uwezo wao, lakini pia katika kuboresha maisha ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania wote,” alisema.

Katika makao makuu ya Afrika Mashariki (EAC), Kaimu Balozi Blaser aliungana na Mkurugenzi wa USAID Kenya na Afrika Mashariki Karen Freeman na Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Liberát Mfumukeko katika kutia saini Makubaliano ya Msaada wa Malengo ya Maendeleo Kikanda (Regional Development Objectives Grant Agreement). Katika makubaliano hayo, Serikali ya Marekani itatoa kiasi cha $194 milioni kwa kipindi cha miaka mitano kwa jumuiya hiyo (EAC) ili kuendeleza malengo ya maendeleo ya pamoja. Baada ya hafla ya utiaji saini, Kaimu Balozi Blaser alitembelea kituo cha shirika la African Wildlife Foundation cha kufundishia mbwa wa kubaini pembe za ndovu (Canine Training Center) kinachofadhiliwa na Serikali ya Marekani. Mbwa hao watapelekwa watakaopelekwa katika bandari na viwanja vya ndege Dar es Salaam na kanda yote ya Afrika Mashariki.

Kwa habari zaidi kuhusu taarifa hii, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani katika simu: Tel: +255 22 229-4000 au baruapepe: DPO@state.gov.