Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam 11 Aprili, 2022 Mkurugenzi Mkuu Lwoga Wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa Wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Walimu na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia Wana habari Wageni waalikwa Mabibi na mabwana Ni heshima kwangu kuwa nanyi hapa asubuhi ya leo, mwanzoni mwa wiki muhimu sana katika historia ya …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 11 Aprili, 2022 | Categories: Tamko
Marekani ina furaha kuchangia na Watu wa Tanzania zaidi ya dozi milioni moja za chanjo dhidi ya Covid-19. Marekani inasaidia kuiongoza dunia katika kulitokomeza janga hili, kujenga dunia iliyo salama zaidi na iliyokingwa zaidi dhidi ya kitisho cha maradhi ya kuambukiza. Nchi zote, bila kujali hali zao za kiuchumi, zinahitaji chanjo zinazokidhi viwango vya juu …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 24 Julai, 2021 | Categories: matukio, Tamko
Katika Maadhimisho ya Miaka 245 ya Uhuru wa Marekani na Miaka 60 ya Uhusiano kati ya Marekani na Tanzania Tarehe 4 Julai, Wamarekani tutaadhimisha miaka 245 ya uhuru wetu. Harakati zetu za kudai uhuru zilichagizwa na amali na maadili kadhaa: Usawa, uhuru, haki za binadamu kwa wote, na kupigania maendeleo, ustawi na heshima kwa watu …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 5 Julai, 2021 | Categories: habari, Tamko
Habari za Asubuhi, Waziri wa Afya Mazrui, Mkurugenzi Mkuu, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani, (WHO) Dr. Andemichael Mwakilishi wa taasisi ya Global Fund- Bw. Nelson Msuya Ndugu Wanahabari Na weheshimiwa wafanyakazi wenzetu wa Kituo cha Uendeshaji Huduma za Dharura za Afya ya Jamii Zanzibar. Nimefurahi sana kuungana nanyi hivi leo katika ufunguzi rasmi wa Kituo cha …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 19 Mei, 2021 | Categories: Tamko
Kwa takriban miaka 30, tarehe 3 Mei ya kila mwaka, dunia imekuwa ikiadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inatupa fursa ya kuenzi nafasi na wajibu muhimu wa vyombo huru vya habari katika kimarishaa na kuhifadhi jamii zilizo huru na kuangazia kazi adhimu inayofanywa na …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 3 Mei, 2021 | Categories: habari, Tamko
26 Februari 2021 Habari zenu. Mimi ni Don Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania. Ningependa kuzungumza nawe kuhusu janga la COVID-19 na namna ambavyo tunaweza kufanya kazi pamoja kuzuia kuenea kwake na kutusaidia sote kubaki salama. Toka kuanza kwa janga la Covid-19, takriban watu milioni mbili na nusu wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu. Janga …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 26 Febuari, 2021 | Categories: habari, Tamko
18 Februari 2021 Jana Tanzania ilimpoteza mmojawapo wa majabali (wa kisiasa). Kwa niaba ya Rais Biden, Serikali ya Marekani, na watu wa Marekani, ninatoa rambirambi zangu za dhati kwa Watanzania wote kwa kuondokewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad. Seif alijulikana sana kwa jina la “Maalim,” jina lililoenzi taaluma yake …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 18 Febuari, 2021 | Categories: habari, Tamko
Nilifika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza zaidi ya miaka 30 iliyopita kufanya kazi ya kujitolea kama daktari na uzoefu huo ulinifanya nijenge heshima na mapenzi ya kina na ya kudumu kwa Tanzania na Watanzania. Ilikuwa ni heshima kubwa sana katika maisha yangu, baada ya miaka mingi, kupewa fursa ya kurejea tena nchini humu kuhudumu …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 22 Oktoba, 2020 | Categories: habari, Tamko
Uendeshaji wa chaguzi zijazo nchini Tanzania utakuwa na matokeo muhimu si kwa Tanzania yenyewe pekee, bali pia kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki. Historia ya Tanzania ya kuendesha chaguzi zinazohusisha vyama vingi inarudi nyuma hadi miaka 25 iliyopita na kuifanya nchi hii kuwa mfano wa kuigwa katika bara hili. Serikali ya Marekani inasisitiza na kuthibitisha …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 1 Oktoba, 2020 | Categories: Tamko
Kwa mara ya kwanza nilitembelea Tanzania zaidi ya miaka 30 iliyopita nilipofanya kazi kama daktari wa kujitolea katika hospitali ya umma huko Zanzibar. Katika kipindi hicho cha majira ya kiangazi ninachokikumbuka sana, niliwatibu watoto waliokuwa wakiugua utapiamlo, malaria, minyoo na kifua kikuu. Lakini pia nilivutiwa mno na watu wa Tanzania; walikuwa wema, wakarimu na wakiwachukulia …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 5 Agosti, 2020 | Categories: habari, Tamko
Ubalozi wa Marekani umesikitishwa na hatua za hivi karibuni za Serikali ya Tanzania za kuminya demokrasia, ikiwa ni pamoja na kuwakamata viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiwa katika vikao vyao vya ndani na kufuta leseni ya gazeti la chama cha siasa cha upinzani. Hatua hizi ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 25 Juni, 2020 | Categories: Tamko
Ubalozi wa Marekani umestushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa Mbunge na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe hapo tarehe 9 Juni. Ubalozi unatoa wito wa kufanyika haraka kwa uchunguzi wa kina na huru na kisha kukamatwa na kushtakiwa kwa wale wote waliohusika katika shambulio hilo. Ubalozi unaliona tukio hili katili na …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 9 Juni, 2020 | Categories: Tamko
Dk. Inmi K. Patterson, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania April 20, 2020 Simulizi za uongozi wa Marekani kwenye mapambano ya dunia dhidi ya Covid -19 ni simulizi za siku kadhaa, miezi na miongo. Kila siku msaada mpya wa kiufundi na vifaa unaotolewa na Marekani huwasili kwenye hospitali na maabara duniani kote. Jitihada …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 21 Aprili, 2020 | Categories: habari, Kaimu Balozi, Tamko
Novemba 27, 2019 Serikali ya Marekani inasikitishwa sana na taarifa za ukiukwaji katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 24. Wasimamizi wa uchaguzi, kwa kiasi kikubwa, waliwatenga wagombea kutoka vyama vya upinzani katika mchakato wa uchaguzi. Hali hii ya mkanganyiko inazua swali kuhusu uhalali wa mchakato wa uchaguzi na matokeo. Msimamo wa Serikali ya Tanzania …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 27 Novemba, 2019 | Categories: Tamko
Taarifa ifuatayo imetolewa kwa pamoja na Ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania. Anza tamko: Ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Uingereza unazidi kusikitishwa na kuongezeka kwa uzorotaji wa mchakato wa haki za raia kisheria nchini Tanzania, kama ilivyojidhihirisha kwa matukio zaidi ya mara kwa mara ya watu kutiwa kizuizini kwa muda bila …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 9 Agosti, 2019 | Categories: Tamko
Ukumbi: Hyatt Regency Hotel Juni 17, 2019 Nakushukuru Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Angela Kairuki, kwa kuanzisha mazungumzo haya na Chama cha Wafanya Biashara wa Marekani nchini Tanzania kwa ushiriki mzuri na mchango wake katika kufanikisha tukio hili. Nimefurahi kuwa hapa pamoja nanyi leo kuzungumzia vigezo muhimu katika kuwezesha mahusiano ya kibiashara …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 18 Juni, 2019 | Categories: Tamko
Ukumbi: Morena Hotel – Dodoma 3 Mei 2019 Ningependa kuungana na wenzangu hapa leo kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia na marafiki wa Marehemu Dr. Reginald Mengi. Katika tulivyosema jana kwenye mitandao ya kijamii, wajibu wa Dr. Mengi katika kuendeleza ukuaji na maendeleo ya Tanzania haupimiki, pia kama ulivyo mchango wake kwa vyombo vya …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 3 Mei, 2019 | Categories: Tamko, Uncategorized
Na Mratibu wa PEPFAR nchini Brian D. Rettmann | Disemba 1, 2018 Miaka kumi na tano iliyopita pale Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI, au kwa kifupi PEPFAR ilipoanza, nchini Tanzania na mahali pengi duniani, kuwa na VVU ilikuwa sawa na hukumu ya kifo. Leo hii, tupo karibu zaidi kulidhibiti janga hili …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 3 Disemba, 2018 | Categories: Tamko
https://www.state.gov/r/pa/prs/ps/2018/11/287242.htm Heather Nauert Msemaji Wa Wizara Ya Mambo Ya Nje Washington, DC Novemba 9, 2018 Serikali ya Marekani imesikitishwa sana na matukio ya mashambulizi yanayoshamiri na hatua za kisheria zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania, ambazo zinakiuka uhuru wa raia na haki za binadamu, na zinazojenga mazingira ya vurugu, vitisho na ubaguzi. Tunahuzunishwa na hatua za ukamataji …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 13 Novemba, 2018 | Categories: Tamko
Marekani imesikitishwa na uendeshaji wa chaguzi ndogo zilizofanyika nchini Tanzania tarehe 12 Agosti 2018. Taarifa za kuaminika zinaonyesha kuwa chaguzi ziligubikwa na vurugu zilizohusiana na uchaguzi, ukiukwaji wa sheria za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kukataa kwa baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwasajili wagombea kutoka vyama vya upinzani, vitisho vya polisi …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 15 Agosti, 2018 | Categories: habari, Tamko
Marekani imesikitishwa sana na taarifa za kutekwa na utumiaji nguvu kikatili uliosababisha kifo cha Daniel John na majeraha kwa Reginald Mallya. Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu. Kuongezeka kwa makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotutia wasiwasi na kutusikitisha sana. Tunatoa wito kwa vyama …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 15 Febuari, 2018 | Categories: Tamko
Na Virginia Blaser – Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania 1 Juni 2017 Kwa kipindi cha miaka minne iliyopita nilipata heshima ya kufanyakazi bega kwa bega na Watanzania, Wamarekani na wabia wengine waliojitoa kwa dhati kutekeleza programu na sera zinazoboresha maisha ya mamilioni ya watu nchini na katika kanda. Kuanzia utoaji huduma za afya kwa …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 2 Juni, 2017 | Categories: Tamko
Tunatambua kwamba hivi karibuni Serikali ya Tanzania imetangaza mabadiliko katika muongozo wa utoaji huduma za kukabiliana na VVU/UKIMWI kwa makundi maalumu yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU na yenye viwango vikubwa zaidi vya maambukizi ya virusi hivyo. Serikali ya Tanzania haijaipatia Serikali ya Marekani taarifa yoyote rasmi kuhusu mabadiliko haya yanayoweza kuathiri programu zinazofadhiliwa …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 21 Febuari, 2017 | Categories: Tamko
Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Mabalozi wa Ubelgiji, Denmark, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Hispania, Sweden, Uingereza na Mabalozi wa Canada, Norway, Uswisi na Marekani wanatoa tamko lifuatalo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Denmark, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Hispania, Sweden, Uingereza na Mabalozi wa Canada, …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 9 Novemba, 2015 | Categories: Tamko
Kwa niaba ya Rais Obama na watu wa Marekani, nawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uchaguzi wa rais na wabunge ulioendelea kuthibitisha rekodi nzuri ya Tanzania katika kujenga demokrasia imara. Wakati Rais John Pombe Magufuli na serikali yake wakichukua majukumu yao, tunatarajia kuendelea na ubia wetu wa karibu na kuimarisha zaidi ushirikiano …
Read More»
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 5 Novemba, 2015 | Categories: Tamko