Kaimu Balozi Wa Marekani Azindua Laini Maalum Ya Simu Kwa Ajili Ya Matibabu Ya VVU/Ukimwi Na Basi Maalumu La Kutoa Huduma La TAYOA

Kaimu Balozi Wa Marekani Azindua Laini Maalum Ya Simu Kwa Ajili Ya Matibabu Ya VVU/Ukimwi Na Basi Maalumu La Kutoa Huduma La Tayoa
Kaimu Balozi Wa Marekani Azindua Laini Maalum Ya Simu Kwa Ajili Ya Matibabu Ya VVU/Ukimwi Na Basi Maalumu La Kutoa Huduma La Tayoa
Kaimu Balozi Wa Marekani Azindua Laini Maalum Ya Simu Kwa Ajili Ya Matibabu Ya VVU/Ukimwi Na Basi Maalumu La Kutoa Huduma La Tayoa

Dar es Salaam, TANZANIA.  Kuelekea siku ya UKIMWI Duniani inayoadhimishwa tarehe 1 Disemba, hapo tarehe 29 Novemba Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Virginia Blaser alitembelea taasisi ya vijana inayojihusisha na mapambano dhidi ya UKIMWI ya Tanzania Youth Alliance (TAYOA) na kuzindua namba maalumu ya simu inayomuezesha mtu yoyote kupiga na kupata ushauri wa kitabibu kuhusu UKIMWI (National Health AIDS Helpline – 117)  pamoja na Basi maalumu la kutolea huduma maeneo mbalimbali. Kaimu Balozi Blaser na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Marekani ya Udhibiti Maradhi (CDC) Dr. David Lowrance walipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA Peter Masika na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Balozi Charles Sanga.

Katika ziara hiyo, Kaimu Balozi Blaser aliweza kushuhudia utendaji wa kituo cha ushauri cha TAYOA kwa njia ya simu. Baada ya kuzindua laini hiyo mpya itakayotumiwa katika kutoa ushauri wa kimatibabu ikiwa ni sehemu Mpango wa Kitaifa wa Huduma ya Ushauri kuhusu UKIMWI kwa Njia ya Simu, Kaimu Balozi aliweza yeye mwenyewe kupokea simu kutoka kwa mteja na kushuhudia jinsi huduma hii inavyotoa msaada mkubwa na majibu sahihi kuhusu matibabu kwa wahitaji. Aidha alishiriki katika kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na kuwezesha ujumbe huo mahsusi kuhusu masuala ya afya kuwafikia watu 500,000.

Hali kadhalika Kaimu Balozi Blaser alifanya majadiliano ya kina na ya wazi na wahudumu 20 wa afya ya jamii yaliyoangazia masuala ya ukatili wa kijinsia na miongozo ya mpango mpya unaoungwa mkono na taifa na Shirika la Afya Duniani (WHO) wa kuwaanzishia matibabu mara moja wale wanaopima na kukutwa na VVU (Test and Start).  “Lengo letu ni kuwa na kizazi kisichokuwa na UKIMWI nchini Tanzania, na itahitaji jitihada zetu sote – serikali, sekta binafsi, wabia, wafadhili na watu wa Marekani wakishirikiana na Watanzania ili kufikia azma hii,” alisisitiza Kaimu Balozi Blaser.

Kwa pamoja na Mkurugenzi wa TAYOA Peter Masika na Mwenyekiti wa Bodi Balozi Charles Sanga, Kaimu Balozi Blaser alikata utepe kuzindua Basi la TAYOA litakalotumika kutoa huduma za matibabu na ushauri kuhusu VVU/UKIMWI katika maeneo mbalimbali. Basi hilo litaiwezesha TAYOA kufikisha huduma hii muhimu kwa jamii ambazo hazifikiwi kwa urahisi nchini Tanzania. Katika mwaka 2016, Serikali ya Marekani kwa kupitia Mpango wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR) na Taasisi ya Kudhibiti Maradhi ya Marekani (CDC) waliipatia TAYOA  kiasi cha Dola za Kimarekani milioni1.8 kwa ajili ya kutoa huduma za upimaji VVU na ushauri kwa jamii zinazohamahama na zile zilizo katika hatari zaidi ya maambukizi nchini.

Kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Marekani kwa simu Namba: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.