Kuzorotoa Kwa Haki Za Kiraia Na Haki Za Binadamu Tanzania

https://www.state.gov/r/pa/prs/ps/2018/11/287242.htm

Heather Nauert
Msemaji Wa Wizara Ya Mambo Ya Nje
Washington, DC
Novemba 9, 2018

Serikali ya Marekani imesikitishwa sana na matukio ya mashambulizi yanayoshamiri na hatua za kisheria zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania, ambazo zinakiuka uhuru wa raia na haki za binadamu, na zinazojenga mazingira ya vurugu, vitisho na ubaguzi. Tunahuzunishwa na hatua za ukamataji watu unaoendelea na unyanyasaji wa makundi maalum, wakiwemo mashoga, na wengine wanaotaka kutumia haki zao za uhuru wa kujieleza, kushiriki na kukusanyika. Vyombo vya kisheria vinatumika kudhibiti uhuru wa raia kwa wote.

Kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania kunakwamisha maendeleo, ustawi wa uchumi,  amani na usalama. Tunatoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuchukua hatua za makusudi kulinda haki za asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya, wanaharakati wa kisiasa na watu wote kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu, na makubaliano ambayo  nchi imeridhia kikanda na kimataifa.