Flag

An official website of the United States government

Marekani na Taasisi ya Jane Goodall Tanzania Yazindua Mradi mpya
Ni wa Maendeleo Endelevu wenye thamani ya dola milioni 30 unaofadhiliwa na USAID
3 MINUTE READ
Novemba 17, 2023

Leo, Marekani na Taasisi ya Jane Goodall (JGI) Tanzania wamezindua rasmi mradi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tumaini Kupitia Vitendo (Hope through Action).

Ukifadhiliwa na watu wa Marekani kupita USAID, mradi huo utasimamiwa na kuongozwa na wazawa kupitia shirika la Jane Goodall tawi la Tanzania. Mradi huo ni matokeo ya uhusiano wa miaka 20 kati ya USAID na Taasisi ya Jane Goodall nchini Tanzania. Katika kipindi cha miaka mitano, mradi wa USAID Tumiani Kupitia Vitendo utapanua kazi ya maendeleo endelevu ya JGI-Tanzania na kurejesha makazi na ulinzi wa hifadhi zilizopo Magharibi mwa Tanzania.

“Ushirikiano huu na Taasisi ya Jane Goodall – Tanzania ni kielelezo kikuu cha dhamira ya USAID ya kuwaweka watandaji wazawa mbele na kukuza maendeleo yanayoongozwa na wazawa,” alisema Mkurugenzi wa USAID wa Ofisi ya Manunuzi Bi. Leslie-Ann Nwokora. “Hongera JGI -Tanzania; hii ni hatua muhimu na USAID inawaunga mkono.”

Mradi wa USAID Tumaini Kupitia Vitendo unaangazia maendeleo ya muda mrefu ili kuboresha maisha ya watu, uzalishaji wa kilimo chenye tija, na usimamizi wa misitu. Unasaidia uwekezaji kwa ajili ya uhifadhi wa kudumu wa misitu, manufaa kwa jamii na mapato dhabiti kwa kuimarisha haki za ardhi., kuboresha usimamizi wa misitu, kukuza kilimo endelevu, kuanzisha malipo ya huduma za mfumo ikolojia, kushughulikia ukatili wa kijinsia, na kusaidia uongozi wa vijana nchi nzima.

Kwa kuzingatia kukabiliana na ustahimilivu wa jamii kwa mabadiliko ya tabia nchi na ulinzi wa viumbe hai, athari za mradi zitawasilishwa kwa takwimu za sasa. teknolojia bunifu ya kijiografia na sayansi, mbinu bora za usimamizi wa maarifa, mawasiliano, na usimulizi za hadithi. Msisitizo zaidi utawekwa kwenye usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa kijamii kupitia ufadhili wa mfuko wa USAID wa Usawa wa Kijinsia na Vitendo vya Usawa.

Magharibi mwa Tanzania ni nyumbani mwa sokwe wengi takribani 2,200 nchini na ni sehemu kubwa ya urithi wa asili wa Tanzania. Changamoto za kiuchumi, kiafya na kielimu zinazowakabili watu wake zimesababisha kuongezeka kwa vitisho vya mabadiliko ya tabia nchi na viumbe hai, hasa mabadiliko yasiyo endelevu ya misitu kwa ajili ya kilimo. Kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, mradi wa USAID Tumiani Kupitia Vitendo (Hope Through Action) unalenga kutatua changamoto hizo.