Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) yaahirisha kupigia kura mkataba wake na Tanzania

MCC Logo

Dar es Salaam, TANZANIA. Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) linalomilikiwa na Serikali ya Marekani ilikutana tarehe 16 Disemba na jana ilitoa tamko linalopatikana katika anuani ya mtandao hapa. Katika tamko hilo, Bodi ya MCC inasema kuwa imeamua kutopigia kura mkataba unaopendekezwa kati ya MCC na Tanzania, ikisubiri kutatuliwa kwa masuala ya kiutawala inayoyatilia shaka na ambayo yanaweza kuipotezea Tanzania sifa ya kuweza kupata msaada wa MCC.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Mtaalamu wa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani.