Tamko la Balozi Mark B. Childress kuhusu uamuzi wa Shirika la Changamoto za Milenia kusitisha ushirikiano na Tanzania

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilikutana tarehe 28 Machi, 2016 na kupiga kura kusitisha mchakato wa maandalizi ya mkataba wa pili na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ninaunga mkono kikamilifu uamuzi huo wa Bodi wa kusitisha maandalizi ya mkataba wa pili.

Marekani na Tanzania tumekuwa na uhusiano wa muda mrefu na wa kina katika sekta nyingi.  Tukiwa mbia mkubwa zaidi wa maendeleo kwa Tanzania, Marekani itaendelea kufanya kazi pamoja na Tanzania katika kuboresha afya na elimu, kukuza uchumi na kuimarisha usalama.

Tamko kamili la Bodi ya MCC linapatikana katika mtandao kupitia anuani ifuatayo:  https://www.mcc.gov/news-and-events/release/stmt-032816-tanzania-partnership-suspended.

Kwa taarifa zaidi kuhusu tamko hili, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam.