Mkurugenzi Mkazi wa USAID Andy Karas Atembelea Miradi Mkoani Kigoma

Dar es Salaam, TANZANIA. Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) nchini Tanzania Andy Karas alifanya ziara mkoani Kigoma kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani mkoani humo pamoja na kuonana na viongozi wa mkoa kutathmini miradi inayolenga kusaidia jitihada za Serikali ya Tanzania katika nyanja za nishati, uhifadhi wa mazingira, huduma za afya ya uzazi na afya ya mtoto, huduma za kubabiliana na malaria na msaada kwa wakimbizi.

“Ni furaha kwangu kutembelea mkoa wa Kigoma,” alipotembea jamii na kituo cha afya kinachofadhiliwa na programu ya afya inayofadhiliwa wa USAID iitwayo Boresha Afya. “Kazi inayofanywa na wabia wetu wa Kitanzania ni ya kupigiwa mfano na yenye kuleta matokeo makubwa. Tuna fahari kushirikiana na Watanzania katika kujenga Tanzania yenye afya, ustawi na usalama zaidi.”

Kwa muda mrefu mkoa wa Kigoma umekuwa mwenyeji wa miradi kadhaa ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa takribani miongo miwili na Taasisi ya Uhifadhi ya Jane Goodall (JGI) katika kuhifadhi na kuboresha ikolojia ya Gombe. Toka wakati huo taasisi ya JGI kwa msaada wa Serikali ya Marekani, imepanua shughuli zake za uhifadhi kwa kujumuisha kufanya kazi na jamii katika miradi ya kiuchumi inayojali mazingira, uzazi wa mpango na ajira.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe:  DPO@state.gov.