Flag

An official website of the United States government

Mradi wa USAID Umeongeza Uwezo wa Tanzania
Kutoa Huduma Bora za Kinga na Tiba ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.
4 MINUTE READ
Oktoba 26, 2023

Leo mjini Dodoma, Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, inaadhimisha miaka minne ya mafanikio ya kuongeza uwezo wa taasisi za serikali na wabia kutekeleza huduma bora za Kinga ya Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto kupitia mradi wa USAID wa Kupunguza Maambukizi wa RISE II unaotekelezwa na mothers2mothers. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Serikali ya Tanzania Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa wakiwemo timu za afya za mikoa na timu za afya za wilaya, Washirika wa Maendeleo, Washirika wa Utekelezaji wa PEPFAR, Asasi za Kiraia, walengwa na wawakilishi kutoka sekta binafsi.

USAID imechangia kupungua kwa vifo vya watoto walioathirika na virusi vya UKIMWI nchini Tanzania kama sehemu ya ushirikiano wa muda mrefu wa serikali ya Marekani na Tanzania katika kukomesha janga la VVU. Tangu mwaka 2003, Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) umetoa zaidi ya dola bilioni 6 za Marekani kusaidia Tanzania kudhibiti janga hili kwa njia ya kinga, upimaji, matibabu na uimarishaji wa mfumo wa afya na hivyo kusababisha kupungua kwa kasi ya vifo vya watoto, huku Tanzania ikikaribia kufikia malengo ya UNAIDS 95-95-95 ya kupambana na VVU. Uwekezaji wa mapema katika afya una manufaa kwa ustawi wa Watanzania katika maisha yao na kufanya jamii kustawi zaidi. Hiki ni kipaumbele kwa serikali zote mbili za Tanzania na Marekani, kama inavyoonyeshwa katika Mpango Mkakati wa USAID Tanzania wa Maendeleo ya watanzania wa miaka mitano.

Kupitia mradi wa RISE II, USAID ilifanya kazi na Wizara ya Afya kuandaa Mwongozo wa kitaifa wa mpango wa uendeshaji na utekelezaji wa afua ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ngazi ya jamii, ili kuwezesha utekelezaji wa huduma hizo zinazotolewa na mama vinara nchini kote na kusaidia utekelezaji wa modeli hiyo katika vituo vinavyopata usaidizi wa PEPFAR na visivyo na usaidizi wa PEPFAR. Kwa kutumia mfumo huu, mradi ulifanikiwa kuweka asilimia 100 ya wajawazito na akina mama wanaonyonyesha wanaoishi na VVU kwenye Tiba ya Kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi katika vituo 10 vilivyokuwa vikipata usaidizi wa mradi. Kutokanan na matokeo haya zaidi ya asilimia 95 ya watoto waliokuwa kwenye hatari ya kuambukizwa VVU walizaliwa bila VVU, na hii inachangia kufikia malengo ya kizazi kisicho na UKIMWI ifikapo 2030.

Maadhimisho haya ni matokeo ya ushirikiano madhubuti ulioongozwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania- TAMISEMI ikiwemo timu ya afya ya mkoa wa Morogoro na timu za afya za wilaya), waheshimiwa wateja wetu, Mama Vinara, watoa huduma za afya katika vituo vyote. ambapo mpango wa m2m ulitekelezwa, washirika wa utekelezaji na kupitia ushirikiano endelevu wa serikali ya watu wa Marekani na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.