Flag

An official website of the United States government

MSAADA WA CHAKULA KUTOKA SERIKALI YA MAREKANI WAKABIDHIWA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO NCHINI TANZANIA
3 MINUTE READ
Disemba 22, 2023

Leo, msaada wa dharura wa kibinadamu uliotolewa na serikali ya Marekani umewasilishwa kwa waathirika wa mafuriko katika mkoa wa Manyara nchini Tanzania. Maafa hayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 89, kuharibu mamia ya ekari za mashamba na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), kupitia usaidizi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) mkoani Manyara, limekabidhi mafuta ya kupikia na kunde ili kusaidia watu 1,491 walioathiriwa na mafuriko hayo.

Pamoja na kuwasili kwa chakula hicho leo mkoani Manyara, USAID, Kituo cha udhibiti na kuzuia Magonj wa (CDC) pamoja na WFP wanaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania zinazoendelea kukabiliana na maafa hayo kaskazini mwa nchi. Serikali ya Marekani inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa usaidizi wa ziada pale utakapohitajika.

Kwa mawasliano zaidi kuhusu taarifa hizi, wasiliana na Ubalozi wa Marekani kitengo cha Mawasiliano kupitia DPO@state.gov