Flag

An official website of the United States government

Naibu Kiongozi Mkuu wa USAID Coleman Atangaza Msaada wa Dola Milioni 10
Ni za kukabiliana na Tatizo la Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania
2 MINUTE READ
Septemba 11, 2023

Tarehe 6 Septemba, Naibu Kiongozi Mkuu wa USAID Isobel Coleman alitangaza uwekezaji mpya wa USAID katika miradi miwili, wenye thamani ya jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 10 ili kulinda ikolojia muhimu na kupunguza gesi ukaa (carbon sinks) nchini Tanzania.

Hii inajumuisha kiwango cha awali cha Dola za Kimarekani milioni 8 kuzindua mradi wa USAID Tumaini Kupitia Vitendo, mradi wa miaka mitano unaoendeshwa kwa ubia na Taasisi ya Jane ili kuimarisha usimamizi bora wa serikali, vijiji na wadau wa maliasili nchini Tanzania; na Dola za Kimarekani milioni 2.1 kuboresha uwezo wa jamii za pwani na wavuvi wa Tanzania kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabia nchi kama sehemu ya mradi unaoendelea wa USAID Heshimu Bahari.

Miradi hii inachangia katika ushiriki wa USAID katika Kongamano la Hali ya Hewa la Afrika ambapo USAID imetangaza msaada wa jumla wa Dola za Kimarekani milioni 34 kusaidia uongozi wa Afrika katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuchangia ukuaji uchumi na ustawi barani kote, ikijumuisha miradi hii miwili.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia: press@usaid.gov