Flag

An official website of the United States government

Kitengo Cha Upelelezo Wa Makosa Ya Jinai Ya Kimataifa (OCI) Chatoa Mafunzo Kuhusu Usalama Wa Viza Na
Kubaini Nyaraka Ghushi
2 MINUTE READ
Julai 26, 2021

DAR ES SALAAM – Zaidi ya wafanyakazi 75 wa makampuni ya kuhudumia mashirika ya ndege ya National Aviation Services (NAS) na Swissport pamoja na wale wa mashirika kadhaa ya ndege, wamepatiwa mafunzo kuhusu alama za usalama katika viza za Marekani na namna ya kuwabaini wanaotumia nyaraka bandia za kusafiria. Mafunzo hayo yalitolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kimataifa (overseas criminal investigation) cha Ubalozi wa Marekani.

NAS na Swissport ni makampuni ya ukandarasi yanayotoa huduma za uwakala wa usalama na ukatishaji tiketi kwa makampuni mbalimbali ya ndege yanayotumia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Mafunzo haya yalilenga kuwapatia wafanyakazi hawa wanaohudumia kampuni za ndege ujuzi wa kubaini nyaraka mbalimbali za kusafiria za kughushi na jinsi wahalifu wanavyozitumia kujaribu kuingia Marekani.

Mafunzo haya ni kielelezo kingine cha ubia imara wa miaka 60 kati ya Marekani na Tanzania.