Hatua Zilizochukuliwa na Serikali ya Marekani Kukabiliana na COVID-19 (3 Aprili, 2020)

Hatua Zilizochukuliwa na Serikali ya Marekani Kukabiliana na COVID-19 (3 Aprili, 2020)

Dar es Salaam: Serikali ya Marekani imejizatiti, na kila siku, kote duniani, inapiga hatua kukabiliana na changamoto ya kihistoria inayotokana na janga la COVID-19. Watu wa Marekani, kupitia taasisi za kiserikali, makampuni binafsi ya kibiashara, mashirika ya kiraia, mashirika ya misaada na vikundi vya kidini wametoa msaada mkubwa kwa waathiriwa wa virusi vya corona katika …

Toleo Jipya – Taarifa kuhusu covid19

Toleo Jipya: Machi 16, 2020 Miadi kwa ajili ya kupata viza zisozo za wahamiaji (Nonimmigrant visa) inaweza kufanyika kwa ajili ya safari za dharura kama inavyoelezwa katika kipengele kinachohusu maswali kuhusu miadi ya visa katika kiunganishi hapo chini. Aidha, kiunganishi hicho kinatoa maelezo ya jinsi ya kufanya uweze kupata miadi ya visa kwa haraka. https://ais.usvisa-info.com/en-tz/niv/information/faqs Kwa …

Taarifa Muhimu Kuhusu COVID19

Toleo Jipya: Machi 3, 2020 Raia wote wa kigeni ambao si wakazi halali wa kudumu wa Marekani na ambao walikuwa katika Jamhuri ya Watu wa China, isipokuwa katika mamlaka maalumu zinazojitegemea za Hong Kong and Macau, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au katika nchi zote za ukanda wa Schengen katika kipindi cha siku 14 kabla …

Ubalozi Wa Marekani Waendesha Mahafali Ya Programu Ya Mafunzo Ya Kiingereza Jijini Tanga Na Zanzibar

Tanga na Zanzibar (Unguja), TANZANIA. Hapo tarehe 15 na 16 Februari, 2020, Ubalozi wa Marekani uliwatunukia vyeti wahitimu 47 wa programu maalumu ya mafunzo ya Kiingereza inayofadhiliwa na Ubalozi huo iitwayo English ‘Access’ Microscholarship Program mjini Tanga (wasichana 13 na wavulana 12) na Unguja – Zanzibar (wasichana 12 na wavulana 10). Wanafunzi hawa wamehitimu mafunzo …

Marekani yasherehekea kumalizika kwa mafunzo ya Askari wa Kikosi cha Kulinda Amani Afrika (APRRP) kwa kukabidhi vifaa kwa JWTZ

Dar es Salaam, TANZANIA.  Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 18 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama sehemu ya Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Afrika (African Peacekeeping Rapid Reaction Program – APRRP). Ubia wa Majeshi ya Kulinda Amani ya …

Ubalozi Wa Marekani Waendesha Mahafali Ya Programu Ya Mafunzo Ya Kiingereza Jijini Mwanza

Mwanza, TANZANIA. Hapo tarehe 1 Februari, 2020, Ubalozi wa Marekani uliwatunukia vyeti wahitimu 25 wa programu maalumu ya mafunzo ya Kiingereza inayofadhiliwa na Ubalozi huo iitwayo English ‘Access’ Microscholarship Program iliyokuwa ikiendeshwa katika Chuo Kikuu cha Mt.Augustine (SAUT) jijini Mwanza.  Wanafunzi hao (wasichana 13 na wavulana 12) waliweza kuhitimu mafunzo ya miaka miwili ya Kiingereza …

Tamko Kuhusu Hakikisho Lililotolewa na Rais Magufuli kuhusu Uchaguzi Huru na wa Haki

Tumetiwa moyo sana na hakikisho lililotolewa na Rais Magufuli hapo tarehe 21 Januari, kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye uwazi pamoja na mwaliko wake kwa waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa. Tunatarajia uchaguzi ambao raia wote na wagombea wa vyama vyote wanaweza kukutana kwa amani, wakielezea mawazo yao na kampeni …

Makabidhiano ya Pikipiki 16 kutoka Serikali ya Marekani kwenda TAMISEMI kwa ajili ya kuboresha huduma za UKIMWI ngazi ya Jamii

Dodoma: Januari 23, 2020, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ilikabidhi pikipiki 16 za Yamaha na makabati 800 kwa ajili ya kuhifadhia faili zenye taarifa muhimu za walengwa, kwa Serikali ya Tanzania. Pikipiki hizi zitatumiwa na watoa huduma ngazi ya kata, kwa ajili ya kufuatilia utoaji wa huduma za …

Great Seal of the United States

Taarifa kuhusu Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania

Muhtasari: PEPFAR ni mpango maalumu wa Serikali ya Marekani wa kusaidia kuokoa maisha ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI duniani kote.  Mpango huu wa kihistoria ni mkubwa zaidi ya mpango wowote uliowahi kuendeshwa na nchi yoyote duniani katika kukabili ugonjwa mmoja kimataifa.  Mpango wa PEPFAR huongozwa na kuendeshwa na majukumu ya pamoja kati ya nchi wafadhili na nchi …