Flag

An official website of the United States government

Serikali ya Marekani yaadhimisha miaka mitano ya ushirikiano na Tanzania katika uwezeshaji wa vijana
2 MINUTE READ
Julai 28, 2022

Julai 28, 2022 – Leo, mjini Dodoma, Mheshimiwa Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID Bi. V. Kate Somvongisiri, wamesherehekea mafanikio ya Mpango wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana. Ukitekelezwa katika mikoa ya Iringa, Mbeya, na Zanzibar, mpango huo wa miaka mitano uliogharimu dola milioni 20 umesaidia vijana wa vijijini wenye umri kati ya miaka 15-35, kujihusisha na biashara ya kilimo na minyororo mingine ya thamani na kuongeza fursa zao za kiuchumi huku wakikuza uongozi na maisha bora.

Vijana wa Kitanzania wana nafasi kubwa katika maendekeo ya uchumi wa nchi yao, lakini kwa vijana 800,000 wanaoingia katika nguvu kazi kila mwaka, ajira bado ni changamoto. Mradi wa Feed the Future Inua Vijana unashughulikia vikwazo hivi kwa kuongeza fursa za kipato kwa vijana kupitia mafunzo ya kitaaluma na kuunganisha vijana na fursa za kazi rasmi na zisizo rasmi.

Mkurugenzi mkazi wa USAID, Bi. V. Kate Somvongsiri, alisema, “Tunajivunia kuwa mradi huu wa Inua Vijana umewafikia zaidi ya vijana 43,000 na kutoa zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni 5.3 ($2.3 milioni) kama ruzuku kwa biashara za kilimo zinazomilikiwa na vijana.” Mkurugenzi aliendelea, “Inua Vijana imewasaidia vijana kupata stadi za maisha, na kuongoza juhudi za maendeleo ya jamii…. Mradi huu umebadilisha mtazamo wa jamii kuhusu vijana na kuwa mawakala wa maendeleo, wenye uwezo wa kubadilisha jamii inayowazunguka.”

Waziri Joyce Ndalichako aliongea na vijana wanufaika wa Inua Vijana waliotoa shuhuda zao za mafanikio ya mradi.