Flag

An official website of the United States government

Serikali ya Marekani yazindua Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Vijana
2 MINUTE READ
Oktoba 31, 2022

Mtwara – Leo, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania, imezindua mradi wa miaka miwili utakaogharimu dola za Marekani milioni 1.2 kwa lengo la kusaidia na kuimarisha ushiriki wa vijana katika mchakato wa utawala wa serikali za mitaa.

Miaka michache ijayo, idadi ya Watanzania itaongezeka zaidi ya watu milioni 10. Wastani wa umri wa mtanzania ni miaka 17.5, na asilimia 44 ya watu ni chini ya umri wa miaka 15. Katika mkoa wa Mtwara pekee, takriban theluthi moja ya wakazi ni vijana. Kama ilivyo duniani kote, vijana wa Mtwara wanakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwa ni upatikanaji wa elimu, ajira pamoja na ushirikishwaji katika jamii zao.

Ukitekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kamati ya Uokoaji, kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mtwara dhidi ya Umaskini, na Mlango wa Matumaini kwa Wanawake na Vijana Tanzania, mradi huu wa Vijana-Kwanza hutambua na kuwawezesha vijana waleta mabadiliko wanaongoza midahalo, kuhamasisha na kuongeza shughuli za uwezeshaji katika jamii zao, na pia kutumika kama kiungo kati ya serikali za mtaa, viongozi wa kimila na madhehebu mbalimbali. Mashirika yanayoongozwa na vijana pia yatawezeshwa kupaza sauti za vijana katika utawala wa serikali za mitaa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Ofisi ya Haki za Demokrasia na Utawala USAID Bw. Bret Saalwaechter alisema, “Ni muhimu vijana kuwakilishwa, kushiriki, na kuongoza jamii zao. Hizi ni juhudi za pamoja, na sina shaka vijana wa Tanzania wako tayari na wana uwezo wa kuchukua jukumu hili la uongozi katika kutumikia nchi.”