Flag

An official website of the United States government

Siku 16 za Harakati za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
6 MINUTE READ
Disemba 11, 2023

Mwaka huu tunaadhimisha miaka 75 tangu kutolewa kwa Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, hati muhimu inayothibitisha kwamba kila binadamu anazaliwa huru na sawa kwa heshima na haki. Tunakubaliana kikaamilifu na tamko hili, na tunatoa wito kwa serikali, jamii, makampuni ya sekta binafsi, na watu binafsi kuungana nasi katika kusaidia kuiunda dunia hiyo – kwa ajili ya jamii zetu leo na kesho. Tazama jinsi Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unavyowekeza katika harakati hizi za kuleta mabadiliko.

Mradi Maelezo
Programu ya Viongozi Kutembelea Marekani kwa Ziara za Kimafunzo (International Visitor Leadership Program) – Edwin Mugambila, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi iitwayo Tanzania Relief Initiatives ameondoka Kwenda Marekani kushiriki Programu ya Kudhibiti Usafirishaji Haramu wa Binadamu (the Combating Trafficking in Persons III)
Mradi wa USAID wa Afya Yangu – Kanda ya Mashariki – Kupitia jukwaa liitwalo JAMVI la Vijana, mijadala ya kijamii imefanyika pamoja na vipindi vya uelimishaji rika (peer to peer sessions) vimefanyika katika shule za msingi na serikali. Vipindi vya redio vimefanyika kujenga ufahamu.
Vituo vya Kimarekani (American Corners) Zanzibar, Pemba, na Dar es Salaam – Vituo hivi viliendesha majadiliano ya jamii yaliyolenga Kujenga Jamii iliyoazimia kukomesha Ukatili wa Kijinsia.
Utekelezaji wa Tuzo Inayotolewa kwa washiriki wa Programu ya IVLP wanaoleta athari chanya kwa jamii zao (IVLP Impact Award) – Batilda Mushi aliendesha warsha “Haki ya Kesi/Mashauri ya Haki” (Right to a Fair Trial) zilizofanyika Dar es Salaam na Arusha.
Mradi wa USAID wa Polisi na Magereza Kusaidia Uboreshaji wa Huduma za Afya Tanzania – Mradi huu uliendesha mafunzo ya siku tano katika eneo la kazi kuhusu ukatili wa kijinsia eneo la kazi kwa wafanyakazi wanahusika na ustawi wa jamii ili kujenga ufahamu, kubaini matukio na namna ya kuyatolea taarifa.
Ubia na WiLDAF uliotangazwa tarehe 5 Desemba, 2023 – “Kutokomeza Kabisa Ukeketaji mkoani Mara – Jamii Imara” – Mradi huu wa miezi 18 unalenga kuchangia kuongeza kasi ya kutokomeza Ukeketaji wa Wanawake nchini Tanzania kama ilivyoaishiwa katika Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Ukeketaji.

 

Lengo La Msingi
Marekani imedhamiria kwa dhati kushughulikia tatizo hili kubwa na gumu linalokwaza uwezo wa waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini Marekani na duniani kote kupata haki zao. Tunatambua uhusiano uliopo kati ya usawa wa kijinsia – ikiwa ni pamoja na kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia – na demokrasia, usalama wa taifa, usalama wa kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, afya ya umma kimataifa na haki za binadamu. Ni kwa sababu hiyo, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Marekani imeweka kipaumbele katika kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Marekani wa Uwiano na Usawa wa Kijinsia na kuboresha Mkakati wa Marekani wa Kuzuia na Kukabili Ukatili wa Kijinsia Kimataifa na Mkakati wa Marekani kuhusu Wanawake, Amani na Usalama.