Tamko La Pamoja Kuhusu Makubaliano Ya Kuendelea Kwa Msaada Wa Maendeleo Wa USAID Kwa Tanzania

USAID - Kutoka Kwa Watu Wa Marekani
USAID - Kutoka Kwa Watu Wa Marekani
USAID – Kutoka Kwa Watu Wa Marekani

Leo tarehe 1 Agosti 2016, Bi Sharon Cromer Mkurugenzi Mkazi akiwakilisha  Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Dk. Servacius Likwelile, akiiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesaini mkataba wa miaka mitano wa msaada wa USAID kwa Tanzania (five-year strategic assistance agreement).  Kwa kupitia mkataba huu, Marekani, kwa uratibu kamili wa Serikali ya Tanzania, inalenga kuisaidia Tanzania kufikia azma yake ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Chini ya mkataba huu, mwaka huu, Serikali ya Marekani kupitia USAID inatarajia kuwekeza nchini Tanzania Dola za Kimarekani milioni 407 katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sekta za afya, kilimo, usimamizi wa maliasili, nishati na utawala wa kidemokrasia.  Uwekezaji huu  wa Dola za Kimarekani milioni 407 ni nusu ya bajeti ya mwaka ambayo  Serikali ya Marekani hutumia kwa maendeleo na miradi mingine ya pamoja nchini Tanzania ambayo baadhi hutekelezwa na Serikali ya Tanzania na mingine hutekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi nchini Tanzania.

 

Kwa taarifa zaidi kuhusu mkataba huu, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam au Bw. Benny Mwaipaja, (bmwaipaja@mof.go.tz), Kaimu Afisa Habari Mkuu wa Serikali – Wizara ya Fedha, Dar es salaam.