Flag

An official website of the United States government

Tamko Kuelezea Masikitiko Yetu Kuhusu Uhuru wa Kujieleza na Ushiriki Jumuishi wa Kisiasa
2 MINUTE READ
Juni 25, 2020

Ubalozi wa Marekani umesikitishwa na hatua za hivi karibuni za Serikali ya Tanzania za kuminya demokrasia, ikiwa ni pamoja na kuwakamata viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiwa katika vikao vyao vya ndani na kufuta leseni ya gazeti la chama cha siasa cha upinzani. Hatua hizi ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha ya vitisho kwa wanachama wa vyama vya upinzani, asasi za kiraia na vyombo vya habari. Haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza ni mambo yaliyojumuishwa na yanayolindwa na Katiba ya Tanzania na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu. Ubalozi wa Marekani unafahari kusaidia na kuunga mkono uhuru wa kujieleza na ushiriki jumuishi wa kisiasa kwa namna zote.