Flag

An official website of the United States government

Tamko Kuhusu Hakikisho Lililotolewa na Rais Magufuli kuhusu Uchaguzi Huru na wa Haki
2 MINUTE READ
Januari 31, 2020

Tumetiwa moyo sana na hakikisho lililotolewa na Rais Magufuli hapo tarehe 21 Januari, kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye uwazi pamoja na mwaliko wake kwa waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa. Tunatarajia uchaguzi ambao raia wote na wagombea wa vyama vyote wanaweza kukutana kwa amani, wakielezea mawazo yao na kampeni zitakazofanyika katika misingi ya usawa.  Tunatoa wito wa kuharakishwa kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura lenye uwazi, kuanzishwa kwa tume huru za uchaguzi na kuteuliwa mapema kwa waangalizi wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wa kuaminika watakaofuatilia uchaguzi kwa kipindi kirefu na kipindi kifupi.