Taarifa ya UVIKO-19

Tahadhari ya Kiafya: Ubalozi wa Marekani Tanzania (06 Decemba 2021)

Mahali: Tanzania

Tukio:  Tarehe 6 Desemba, Kituo cha Marekani cha Udhibiti wa Maradhi (CDC) kitatekeleza sharti la wasafiri wote walio na umri wa zaidi ya miaka miwili wanaoingia Marekani wawe wamepima UVIKO-19 ndani ya siku moja kabla ya kusafiri.  Bila kujali kama amechanja ama la na bila kujali uraia wake, kila mtu anayeingia Marekani ni lazima aonyeshe cheti cha kutokuwa na UVIKO-19 kutokana na kipimo kilichofanyika siku moja kabla ya kupanda ndege kwenda Marekani. Ni lazima uonyeshe cheti chenye majibu kwamba hujaambukizwa UVIKO-19 kabla hujapanda ndege.

Iwapo umepona UVIKO-19 hivi karibuni, unaweza kusafiri na nyaraka zinazoonyesha kuwa umepona ugonjwa huo (kwamba umeonekana kutokuwa na UVIKO-19 katika vipimo vilivyofanywa si zaidi ya siku 90 kabla ya kuanza safari kutoka katika nchi ya kigeni pamoja na barua kutoa kwa mtoa huduma ya afya mwenye leseni au afisa wa afya ya umma akieleza kuwa umepewa ruhusa ya kusafiri).

Masharti haya ni kwa wasafiri wote wa njia ya anga wenye umri wa miaka miwili au zaidi wanaosafiri kutoka nchi ya kigeni kwenda Marekani.

Hatua za kuchukua:

  • Tembelea Tovuti ya CDC ili kupata taarifa za hivi punde.
  • Kwa taarifa kuhusu hatua unazoweza kuchukua kupunguza hatari ya kuambukizwa UVIKO-19, tafadhali angalia Mapendekezo mapya ya CDC.
  • Tembelea COVID-19 crisis page on travel.state.govkwa taarifa mahsusi kuhusu nchi mbalimbali zinazohusiana na UVIKO-19.
  • Wasiliana na shirika lako la ndege, kampuni ya meli au wakala wako wa safari kuhusu taarifa mpya kuhusu mipango yako ya safari ikiwemo masharti utakayohitajika kuyatimiza kuhusu chanjo na kupima UVIKO kwa nchi utakazopitia katika safari yako.
  • Tembelea tovuti ya Ubalozi wa Marekani kuhusu UVIKO-19 kwa taarifa zaidi kuhusu hali ilivyo nchini Tanzania.

Msaada:
U.S. Embassy Dar es Salaam, Tanzania
686 Old Bagamoyo Road, Msasani,