Tamko Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Novemba 27, 2019

Serikali ya Marekani inasikitishwa sana na taarifa za ukiukwaji katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 24.  Wasimamizi wa uchaguzi, kwa kiasi kikubwa, waliwatenga wagombea kutoka vyama vya upinzani katika mchakato wa uchaguzi.  Hali hii ya mkanganyiko inazua swali kuhusu uhalali wa mchakato wa uchaguzi na matokeo.  Msimamo wa Serikali ya Tanzania kukataa kutoa vibali kwa wakati kwa waangalizi wanaokubalika na mashirika yenye uzoefu kunapoteza Imani Zaidi katika mchakato mzima.