Tamko kutoka Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania

Ubalozi wa Marekani unafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi nchini kote Tanzania. Tunaendelea kufuatilia zoezi la majumuisho ya kura, ikiwa ni pamoja na zoezi linaloendelea la  majumuisho ya kura za urais wa Zanzibar linalofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Tunatoa wito kwa mchakato huu kukamilishwa kwa wakati na kwa uwazi. Aidha, tunatoa wito kwa maafisa wote wa serikali kuheshimu wajibu wa waangalizi rasmi wa uchaguzi kwa kuwaruhusu bila kipingamizi chochote kuangalia vipengele vyote vya mchakato wa uchaguzi. Tunazisihi pande zote husika kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakuwa wa uwazi, huru na wa amani.