Tamko la Pamoja Kuhusu Wasiwasi wa Kuzorota Kwa Haki za Raia Kisheria Nchini Tanzania

Taarifa ifuatayo imetolewa kwa pamoja na Ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania.

Anza tamko:

Ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Uingereza unazidi kusikitishwa na kuongezeka kwa uzorotaji wa mchakato wa haki za raia kisheria nchini Tanzania, kama ilivyojidhihirisha kwa matukio zaidi ya mara kwa mara ya watu kutiwa kizuizini kwa muda bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za sheria nchini. Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni — jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki, la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za kiuchunguzi Bw. Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali za kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai.

 

Tunaisihi Serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake, kama ilivyotambua kwamba ni haki ya msingi na kuridhia kwenye mikataba mbalimbali ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, miongoni mwao ikiwemo Azimio la Kimataifa la Haki za Raia na Kisiasa.

Maliza tamko.