Tangazo la Fursa ya Fedha: Program ya Kiingereza ya Access


Ofisi ya Kingereza, kanda ya Afrika Mashariki na Kati iliyopo Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam, Tanzania, inatangaza shindano la wazi la andiko kwa ajili ya fursa ya fedha ya kuendeshea program ya Access, ambayo inatoa mafunzo ya Kiingereza kwa wanafunzi wenye hali duni kati ya umri wa miaka 13 hadi 20.

Fedha zitakazotolewa ni kwa ajili ya wanafunzi 25 kwa kila darasa kuhudhuria madarasa ya kiingereza yatakayofanyika baada ya muda wa masomo pamoja na shughuli za kuwakuza wanafunzi hao kitaaluma, kwa gharama isiyozidi dola za Kimarekani 25,000 kwa darasa. Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na nje ya nchi pamoja na taasisi za kielimu zinaweza kutuma maandiko kwa ajili ya kuunda, kuendesha, kusimamia na kutathmini madarasa ya Access hapa Tanzania. Taasisi moja inaweza kuomba madarasa mengi ila kiwango cha ukomo kwa maombi ya fedha ni dola za Kimarekani 80,000.

Kwa taarifa zaidi au kutuma maombi, tuma baruapepe kwa relodar@state.gov. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/06/2018.