Wanafunzi wa Sekondari wa Kitanzania warejea kutoka ziara ya kimasomo ya mwaka mmoja nchini Marekani

Tanzanian secondary school students who recently returned from a year-long academic exchange in the United States share a light moment with U.S. Embassy Regional English Language Officer Scott Chiverton.
Wanafunzi wa Sekondari wa Kitanzania warejea kutoka ziara ya kimasomo ya mwaka mmoja nchini Marekani (Picha kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani)
Wanafunzi wa Sekondari wa Kitanzania warejea kutoka ziara ya kimasomo ya mwaka mmoja nchini Marekani (Picha kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani)

Dar es Salaam, TANZANIA.  Wanafunzi 19 wa shule za sekondari wa Kitanzania waliomaliza ziara yao ya mwaka mmoja ya mabadilishano ya kimasomo nchini Marekani hivi karibuni, wiki hii wametembelea Ubalozi wa Marekini jijini Dar es Salaam na kupokewa na Balozi Mdogo wa Marekani nchini Virginia M. Blaser.  Katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, wanafunzi hawa kutoka mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Zanzibar walisoma katika shule za sekondari za Marekani chini ya programu mabadilisho na mafunzo ya vijana inayofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani  iitwayo  Kennedy-Lugar Youth Exchange and Study program (YES).  Vijana hawa walisoma katika shule za sekondari katika majimbo ya California, Connecticut, Georgia, Indiana, Iowa, Michigan, Missouri, Montana, Ohio, Pennsylvania, Texas, Washington na Wisconsin.

Programu ya YES ilianzishwa na Kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mwezi Oktoba mwaka 2002. Toka mwaka 2007 jumla ya vijana wa Kitanzania 150 wameshiriki katika programu hii.  Programu ya YES hutoa msaada wa gharama za mafunzo (scholarships) kwa wanafunzi wa ngazi ya juu ya sekondari (wenye umri wa kati ya miaka 15-17) kwenda Marekani kwa mafunzo ya mwaka mmoja katika shule za sekondari nchini humo. Wanafunzi hawa huishi na familia za Kimarekani, hushiriki katika shughuli mbalimbali ili kujifunza kuhusu jamii ya wamarekani na utamaduni wake, kupata ujuzi wa masuala ya uongozi na kuwaelimisha Wamarekani kuhusu nchi zao na utamaduni wao.  Takriban wanafunzi 900 duniani kote huenda Marekani kila mwaka kupitia programu hii.

Kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam.