Flag

An official website of the United States government

Serikali ya Marekani imejitolea kuunga mkono serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kupambana na janga la
UVIKO-19
4 MINUTE READ
Septemba 10, 2021

DODOMA – Kutoka Dodoma, serikali ya Marekani kupitia shirika lake la maendeleo ya kimataifa (USAID) imezindua rasmi mradi wa kuimarisha usimamizi wa matibabu ya wagonjwa wa UVIKO-19 katika hospitali za rufaa za mikoa. Waliohudhuria katika uzinduzi huu ni  mkurugenzi wa masuala ya dharura na utayari Dkt Elias Kwesi, na mganga mkuu wa serikali Dkt Aifello Sichalwe. Mradi huu mpya unakusudia kuhakikisha vituo vya afya vinatoa huduma bora kwa wagonjwa wote wa UVIKO-19 wenye uhitaji maalum, kwa lengo  kuimarisha  afya zao kwa uharaka… Mradi huu utaimarisha uwezo wa watoa huduama katika kuhudumia wagonjwa hawa kwa ufanisi na ubora katika kutoa huduma endelevu za UVIKO-19.

UVIKO-19 ni janga la dharura la dunia lililokuja na changamoto nyingi zisizotarajiwa na zinzaobadilika kila wakati katika sekta ya afya.

Serikali ya Marekani imeamua kufanya kazi bega kwa bega na serikali ya Tanzania kwa kusaidia  mpango wake wa kitaifa wa kukabiliana na janga la UVIKO-19. Hii ni pamoja na kushirikiana na wadau wote katika sekta ya afya Tanzania kupunguza athari zinazotokana na  janga hili katika kuhakikisha afya na usalama wa jamii nzima. Pamoja na kupunguza athari za janga hilo kwa jamii, upatikanaji sawa na utoaji wa chanjo za UVIKO-19, kupunguza athari za ugonjwa na vifo vitokanayo na UVIKO-19, shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID) pia litasaidia kuzuia na kupunguza athari za UVIKO-19 kwenye miradi ya VVU/UKIMWI na wanufaika wake. Hadi sasa shirika limewekeza jumla ya dola milioni 25.1 za kimarekani katika maeneo haya.

Mradi huu wa wa miezi wenye thamani ya dola 750,000 za Kimarekani, utatekelezwa katika hospital nne za rufaa za mkoa ya:  Hospital ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, hospital ya rufaa ya mkoa Tanga ( Hospitali ya Bombo) , hospital ya rufaa ya Mkoa wa  Arusha (Hospitali ya Mount Meru ) hospital ya rufaa ya Mkoa wa Mwanza ( Hospitali ya Sekou Toure)n. Na  utatekelezaji wake utafanywa  na shirika la kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu (Save the Children). Msaada huu utasaidia utoaji wa vifaa vya tiba ya gesi ya oksijeni na mafunzo kwa watoa huduma za afya. Mafunzo yatazingatia matumizi sahihi na utunzaji wa vifaa hivi  ili kutoa huduma bora na kupanua wigo kwa wagonjwa wa UVIKO-19 wenye shida ya mfumo wa upumuaji. Mafunzo haya pia yatajumuuisha uandaaji na usambazaji wa miongozo kazini iliyohidhinishwa kitaifa, na ufuatiliaji wa tiba ya oksijeni baada ya kuondoka kwa wakufunzi.

Akizungumza katika uzinduzi wa leo, mtaalamu na msimamizi wa miradi ya shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa, Dkt Miriam Kombe alisema “msaada huu ni pamoja na kupunguza athari za janga hilo kwa jamii, upatikanaji sawa na utoaji wa chanjo za UVIKO-19, kupunguza magonjwa na vifo vitonavyo na UVIKO-19 na kuzuia na kupunguza athari za UVIKO-19 kwenye program zetu za usaidizi ya UKIMWI na walengwa.”

Dkt Kombe aliendelea “janga la UVIKO-19 ni miongoni mwa changamoto kubwa kwa afya, ustawi, na usalama wa kiuchumi kwa jamii nzima. Lazima tushirikiane kulishugulikia kwa haraka.”