Toleo Jipya – Taarifa kuhusu covid19

Toleo Jipya: Machi 16, 2020

Miadi kwa ajili ya kupata viza zisozo za wahamiaji (Nonimmigrant visa) inaweza kufanyika kwa ajili ya safari za dharura kama inavyoelezwa katika kipengele kinachohusu maswali kuhusu miadi ya visa katika kiunganishi hapo chini. Aidha, kiunganishi hicho kinatoa maelezo ya jinsi ya kufanya uweze kupata miadi ya visa kwa haraka. https://ais.usvisa-info.com/en-tz/niv/information/faqs

Kwa mujibu wa Tamko la Rais, raia wote wa kigeni ambao si wakazi halali wa kudumu wa Marekani na ambao walikuwa katika Jamhuri ya Watu wa China, isipokuwa katika mamlaka maalumu zinazojitegemea za Hong Kong and Macau, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au katika nchi 26 zinazounda ukanda wa Schengen, Uingereza, isipokuwa nchi zilizochini ya milki ya Uingereza zilizo nje ya bara la Ulaya, Ireland ya Kaskazini na Jamhuri ya Ireland katika kipindi cha siku 14 kabla ya kuwasili kwao nchini Marekani, wamezuiwa kuingia nchini Marekani.  Iwapo unaishi, umetembelea hivi karibuni au unatarajia kutembelea au kupitia China, Iran au nchi yoyote ya ulaya ya ukanda wa Schengen (ambazo ni Austria, Ubelgiji,  Jamhuri ya Czech, Denmark, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Hungary, Iceland, Italy, Latvia, Liechtenstein, Lithuania, Luxembourg, Malta, Uholanzi, Norway, Poland, Ureno, Slovakia, Slovenia, Hispania, Sweden, na Uswisi), Uingereza, isipokuwa nchi zilizo chini ya himaya ya Uingereza nje ya bara la Ulaya, au Jamhuri ya Ireland kabla ya kupanga safari ya kwenda Marekani, unashauriwa kuahirisha miadi yako ya mahojiano kwa ajili ya kupata Viza hadi itakapofika siku 14 kabla ya tarehe ya kuondoka katika nchi hizo.