Flag

An official website of the United States government

Ubalozi wa Marekani wawawezesha wanawake Mwanza kwa kuwapatia stadi za ujasiriamali.
2 MINUTE READ
Julai 20, 2021

Tarehe 19 Julai, Ubalozi wa Marekani ulizindua programu ya Mafunzo kwa Wajasiriamali Wanawake (AWE) jijini Mwanza. AWE ni Programu inayoongozwa na Ikulu ya Marekani ikilenga kuinua maendeleo na ustawi wa wanawake kwa kuwasaidia wanawake wajasiriamali duniani kote. Wanawake 13 wa Kitanzania watashiriki katika mafunzo ya wiki 13 yatakayotolewa kwa njia ya mtandao na kuendeshwa na SELFINA taasisi mbia wa programu ya mabadilishano inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani. Programu ya AWE jijini Mwanza ni programu ya nne ya mpango huo kuendeshwa nchini Tanzania. Mikoa mingine iliyofaidika na mafunzo hayo ni Dar es Salaam, Iringa na Zanzibar. Malengo ya programu hii inayofanyika katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine ni kuwajengea uwezo wanawake kwa kuwapatia stadi na fursa za kufanikiwa kama wamiliki wa biashara.

Ufunguzi wa mafunzo hayo ulifanywa na Kaimu Afisa wa Mambo ya Umma wa Ubalozi wa Marekani Bi. AmyLyn Raynolds na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula.