Flag

An official website of the United States government

Ubalozi Wa Marekani Waendesha Mahafali Ya Programu Ya Mafunzo Ya Kiingereza Jijini Tanga Na Zanzibar
9 MINUTE READ
Febuari 17, 2020

Tanga na Zanzibar (Unguja), TANZANIA. Hapo tarehe 15 na 16 Februari, 2020Ubalozi wa Marekani uliwatunukia vyeti wahitimu 47 wa programu maalumu ya mafunzo ya Kiingereza inayofadhiliwa na Ubalozi huo iitwayo English Access Microscholarship Program mjini Tanga (wasichana 13 na wavulana 12) na Unguja – Zanzibar (wasichana 12 na wavulana 10). Wanafunzi hawa wamehitimu mafunzo ya miaka miwili ya Kiingereza ambapo walihudhuria madarasa ya lugha hiyo mara mbili kwa wiki baada ya muda wa kawaida wa masomo. Katika madarasa hayo, wanafunzi hao walijifunza pia maendeleo ya jamii na stadi za kuijumuisha jamii.Ubalozi wa Marekani unafadhili madarasa haya katika maeneo mengine manne nchini Tanzania ambayo ni MbeyaLindi, Mwanza na PembaMwanzoni mwa mwezi Aprili 2020, ubalozi utafungua madarasa zaidi katika miji ya Tanga, Unguja, na Mwanza.

Akizungumza katika mahafali hayo, Afisa wa Ubalozi wa Marekani anayeshughulikia masuala ya lugha ya Kingereza kwa nchi za Africa ya Mashariki na KatiGeorge M. Chinnery aliwapongeza wahitimu wa Programu ya Access kwa kujitoa kwao kwa dhati na kujifunza kwa bidiiKupitia programu hii, sio tu mmeweza kupata umahiri wa lugha ya Kiingereza bali pia mmekuwa viongozi na mfano wa kuigwa katika jamii. Kupitia miradi ya kujitolea, mmetumiashauku ileile iliyowaletea mafanikio katika masomo, na kuitekeleza katika maisha yenu ya kila siku majumbani mwenu na kwenye jamii nzima. Mahafali hii ya leo ni hatua nyingine katika safari yenu ya kufikia juu zaidi na zaidi kuliko hapo awali.” Katika mahafali hayo, wanafunzi waliwasilisha kazi za kuhudumia jamii walizozifanya wakati wa mafunzo yao kwa lugha ya Kiingereza.

Programu ya Access hutoa mafunzo ya msingi ya lugha ya Kiingereza kwa watoto wenye vipaji kuanzia miaka 13 hadi 20 kutoka jamii zenye hali duni kiuchumi kupitia madarasa yanayoendeshwa baada ya muda wa shule na yanayotoa mafunzo ya kina kipindi cha likizo. Programu ya Access huwapatia washiriki wake stadi za lugha ya Kiingereza jambo ambalo huwapa fursa zaidi za kielimu na ajira. Washiriki pia hujijengea uwezo wa kushindana na kushiriki program za mabadilishano na elimu ya juu nchini Marekani hapo baadae. Toka mwaka 2004, zaidi ya wanafunzi 400 kutoka Tanzania na 150,000 kutoka zaidi ya nchi 85 wameshiriki katika programu hii. Kwa maelezo zaidi, tembelea: https://americanenglish.state.gov/.