Ubalozi wa Marekani wazindua filamu fupi kuhusu ulinzi wa wanyamapori Tanzania

selous012115-059_600pxKatika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanyamapori, tarehe 3 Machi 2015, Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam leo hii umezindua filamu fupi inayoangazia umuhimu wa hifadhi ya wanyamapori nchini Tanzania na haja ya kuongeza jitihada za kukabiliana na ujangiliĀ  na uhifadhi wa wanyamapori. Filamu hii inapatikana katika tovuti ya YouTube kwa anuani ifuatayo https://www.youtube.com/watch?v=rwSVt4tkb0Q, na katika ukurasa wa Facebook wa Ubalozi: https://www.facebook.com/tanzania.usembassy