Flag

An official website of the United States government

Marekani yasherehekea kumalizika kwa mafunzo ya Askari wa Kikosi cha Kulinda Amani Afrika (APRRP)
kwa kukabidhi vifaa kwa JWTZ
3 MINUTE READ
Febuari 4, 2020

Dar es Salaam, TANZANIA.  Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 18 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama sehemu ya Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Afrika (African Peacekeeping Rapid Reaction Program – APRRP).

Ubia wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Afrika au APRRP, ni ubia kati ya Marekani na nchi sita za Kiafrika ambazo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Senegal na Ghana wenye lengo la kujenga uwezo na utayari wa kutoa msaada wa kiuongozi na vifaa kwa oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU). Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, wakufunzi wa Kimarekani wamekuwa wakifanya kazi na kikosi cha JWTZ ambacho ni sehemu ya Kikosi cha Kimataifa cha Kulinda Amani ili kukijengea uwezo wa kushiriki katika oparesheni za kulinda amani, utoaji misaada ya kibinadamu na huduma wakati wa majanga iwe nchini Tanzania na barani kote.

“Marekani itaendelea kuwa mbia imara wa JWTZ,” alisema Kaimu Balozi Patterson katika hafla ya makabidhiano, na kuongeza kuwa “tutaendelea kukisaidia Kikosi cha Kulinda Amani cha Afrika (APRRP) pamoja na mafunzo ya awali ya Askari walinda amani wa Kitanzania.”