Serikali ya marekani yatoa mafunzo ya kiuchunguzi kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa wanyamapori tanzania

Serikali ya marekani yatoa mafunzo ya kiuchunguzi kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa wanyamapori tanzania
Serikali ya marekani yatoa mafunzo ya kiuchunguzi kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa wanyamapori tanzania
Serikali ya marekani yatoa mafunzo ya kiuchunguzi kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa wanyamapori tanzania

Dar es Salaam, TANZANIA.  Kuanzia Desemba 5-8, Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Idara ya Marekani inayoshughulikia Huduma za Uvuvi, Wanyamapori na Ofisi ya Usimamizi wa Sheria (the U.S. Fish and Wildlife Service (FWS) Office of Law Enforcement) ilifanya mafunzo ya vitendo kuhusu uchunguzi wa matukio ya uhalifu kwa wanyamapori katika Chuo cha Polisi Dar es Salaam.

Lengo lilikuwa kutoa ujuzi zaidi ili kukabiliana na ujangili wa wanyamapori na mitandao ya usafirishaji wa nyara Tanzania.

Walioshiriki mafunzo hayo ni pamoja na watu waliomo kwenye kitengo cha taifa na kimataifa cha uchunguzi wa makosa makubwa (National and Transnational Serious Crimes Investigation Unit (NTSCIU), Jeshi la Polisi Tanzania, na ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai (DPP), pamoja na wapelelezi kutoka idara ya wanyamapori katika wizara ya maliasili na utalii na maafisa wengine.

Kwa kuzingatia utaratibu wa uchunguzi wa matukio ya kihalifu, kozi hiyo iliwafundisha washiriki jinsi ya kukabiliana na tukio la kihalifu kwa wanyamapori, na mfunzo ya kukusanya ushahidi, kuimarisha mnyororo wa usimamizi, uhifadhi wa hati, pamoja na maeneo mengine.

Aidha, Serikali ya Marekani ilitoa msaada wa vifaa kumi vya kusaidia ukusanyaji wa ushahidi kwa mashirika yaliyoshiriki katika kozi, kila kifaa kilijumuisha kamera, vifaa vya kupima vinasaba (DNA sample collection kits), vifungashio vya ushahidi na vinginevyo.

Kozi hiyo ya uchunguzi inawakilisha sehemu moja ya mpango mpana na mkubwa wa Serikali ya Marekani wa kupambana na usafirishaji wa wanyamapori.

Kozi hiyo, iliyofanyika pia Uganda kuanzia Novemba 28-Desemba 2, iliandaliwa baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani kufanya tathmini ya usafirishaji wa wanyamapori mwaka 2015 na kubaini umuhimu wa kuanzisha utaratibu wa udhibiti wa matukio ya kihalifu Afrika Mashariki.

Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation lilisaidia utekelezaji wa mradi na kufadhili kozi hiyo kipindi cha nyuma, pamoja na FWS, mwezi Mei 2016.

Kwa habari zaidi kuhusu taarifa hii, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani katika simu: Tel: +255 22 229-4000 au baruapepe: DPO@state.gov.