Marekani na Jumuiya ya Afrika Mashariki Zatia Saini Makubaliano ya Ushirikiano wa $194 Milioni Kuimarisha Maendeleo ya Kikanda

Arusha, TANZANIA. Leo, Serikali ya Marekani na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamezindua Makubaliano ya Msaada wa Malengo ya Maendeleo Kikanda (Regional Development Objectives Grant Agreement) katika mako makuu ya EAC huko Arusha, Tanzania. Kwa niaba ya Serikali ya Marekani, Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID) litachangia kiasi cha $194 milioni kwa kipindi cha miaka mitano kwenye malengo ya maendeleo ya pamoja, kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika haya mawili.

Kiasi cha $30 milioni zitaisaidia moja kwa moja Sekretarieti ya EAC Secretariat, ilhali kitakachobaki kitagharamia wadau wengine wa kikanda katika juhudi zao za kuendeleza ajenda ya EAC ya utangamano kikanda.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania na EAC Virginia Blaser, Mkurugenzi wa USAID wa Kenya na Afrika Masharika Karen Freeman, na Katibu Mkuu wa EAC Balozi Liberát Mfumukeko walitia saini hati ya makubaliano.

Marekani na Jumuiya ya Afrika Mashariki Zatia Saini Makubaliano ya Ushirikiano wa $194 Milioni Kuimarisha Maendeleo ya Kikanda
Marekani na Jumuiya ya Afrika Mashariki Zatia Saini Makubaliano ya Ushirikiano wa $194 Milioni Kuimarisha Maendeleo ya Kikanda

Kaimu Balozi Blaser alitambua manufaa makubwa ya kukuza ushirikiano wa kikanda, akielezea kuwa Marekani inaunga mkono “serikali na mashirika ya kikanda kama EAC katika juhudi zao za pamoja kufungua fursa zilizopo za kikanda kwa manufaa ya watu wake,”

Mkurugenzi wa USAID Freeman alisisitiza mafanikio ya pamoja ya EAC na USAID katika miongo miwili iliyopita. “Kwa kurahisisha utaratibu wa forodha na mipaka, tumerahisisha kasi, gharama nafuu na biashara ya uhakika. Tumeongeza uwekezaji kwa kufanikisha mikataba ya kimataifa ambayo inakuza viwanda vya ndani na vya uzalishaji.”

Kwa makubaliano haya, jumuiya ya EAC na Marekani zitafanya kazi kwa pamoja kwa (i) kuendeleza utangamano wa kiuchumi kikanda, (ii) kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi wanachama na Marekani, (iii) kuboresha usimamizi endelevu wa maliasili katika Ziwa Victoria na mfumo wa ikolojia wa Mto Mara, (iv) kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya ya pamoja maeneo ya mipakani na (iv) kuimarisha mpangilio wa uongozi wa EAC.

Kupata taarifa zaidi kuhusu taarifa hii, tafadhali wasiliana na Ubalozi wa Marekani Ofisi ya Habari simu: +255-22-229-4000 au baruapepe: DPO@state.gov.