Flag

An official website of the United States government

Serikali ya Marekani yakabidhi vifaa vya kusaidia upimaji wa wingi wa virusi vya Ukimwi kwenye damu,
utambuzi wa mapema wa VVU kwa watoto wachanga
4 MINUTE READ
Septemba 15, 2021

Dodoma-Leo, katika viwanja vya makao makuu ya magereza yaliyopo eneo la Msalato, mkoani Dodoma, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi, imekabidhi vifaa vya maabara vyenye thamani ya Shilingi za Tanzania 497,559,000 (Dola za Marekani 216,330) kwenda vituo vya afya kumi na nne (14) vya jeshi la Polisi na Magereza Tanzania vilivyopo mkoani Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Tanga, na Zanzibar. Vifaa hivyo vitaboresha utoaji wa huduma za maabara katika upimaji wa wingi wa VVU mwilini, upimaji wa maambukizi ya VVU kwa watoto wachanga na upimaji wa kifua kikuu. Inatarajiwa kuwa matumizi ya mashine za GeneXpert na hadubini zitachangia kuongezeka kwa kutambua visa vya TB na kupatiwa kwa matibabu kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji, wa shirika   la Tanzania Health Promotion Support (THPS), linalotekeleza mradi wa kudhibiti UKIMWI na kifua kikuu upande wa Polisi na Magereza, Dk. Redempta Mbatia, alimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene, vifaa vilipokelewa kwa niaba ya vituo vya afya vilivyofadhiliwa. Vifaa vilivyotolewa vitawekwa katika vituo vya afya vyenye kiwango cha juu cha wagonjwa na uwezo duni wa uchunguzi.

Kulingana na Utafiti wa Athari za VVU Tanzania (THIS) za mwaka 2017, maambukizi ya VVU ni 4.9% kati ya watu wa miaka 15 na zaidi. Wafungwa wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa Kifua Kikuu na VVU kwa sababu ya mazingira yao, na mienendo hatarishi kati ya makundi ya watu, n.k. wanaouza miili, na watu wanaojidunga madawa ya kulevya. Kabla ya ufadhili huu, kati ya vituo 64 vya afya vilivyofadhiliwa, kumi tu (10) vilikuwa na mashine za GeneXpert; hutumika zaidi kwa uchunguzi wa kifua kikuu, na tisa (9) walikuwa na hadubini za iLED kwa uchunguzi wa kifua kikuu. Hii inasababisha upimaji mdogo wa upimaji wa virusi vya UKIMWI kati ya WAVIU katika vituo vya afya vinavyofadhiliwa na visa kidogo katika utambuzi wa Kifua Kikuu katika jamii.  Mradi wa Polisi na Magereza wa USAID utalenga utambulisho wa WAVIU kupitia upimaji wa wenzi, kubadilisha njia bora za kufubaza makali ya virusi, matumizi ya dawa ya miezi mingi, kufubaza makali ya virusi, kutambua visa vya Kifua Kikuu, na uzuiaji wa Kifua Kikuu. Matokeo ya kukabidhi vifaa, zaidi ya WAVIU 16,000 katika vituo vya afya vya polisi 64 na vituo vya afya vya polisi na magereza watanufaika na matibabu bora.

Akizungumza katika hafla hio leo, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) V. Kate Somvongsiri alisema “Mashine 10 za GeneXpert na hadubini 10 za ILED zilizotolewa leo ni sehemu ya kujitolea kwa USAID, kupitia rasilimali kutoka kwa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI, kuunga mkono dira hii. Vifaa hivi vitaongeza uwezo wetu wa kutoa mipango kamili ya kuzuia VVU, matunzo, na matibabu, na Kifua Kikuu nchini Tanzania.”