Serikali Ya Marekani Yawezesha Mazungumzo Ya Moja Kwa Moja Kati Ya Wasichana 50 Wa Kitanzania Na Mke Wa Rais Michelle Obama Kuhusu Elimu Kwa Wasichana

Serikali Ya Marekani Yawezesha Mazungumzo Ya Moja Kwa Moja Kati Ya Wasichana 50 Wa Kitanzania Na Mke Wa Rais Michelle Obama Kuhusu Elimu Kwa Wasichana
Serikali Ya Marekani Yawezesha Mazungumzo Ya Moja Kwa Moja Kati Ya Wasichana 50 Wa Kitanzania Na Mke Wa Rais Michelle Obama Kuhusu Elimu Kwa Wasichana
Serikali Ya Marekani Yawezesha Mazungumzo Ya Moja Kwa Moja Kati Ya Wasichana 50 Wa Kitanzania Na Mke Wa Rais Michelle Obama Kuhusu Elimu Kwa Wasichana

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike hapo tarehe 11 Oktoba, wawakilishi Serikali ya Marekani na wale wa Shirika la Plan International  waliungana na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama, Mwanamuziki Mahiri wa Kitanzania Vanessa Mdee na Wasichana wa Kitanzania  50 katika mjadala maalumu kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.

Mama Michelle Obama aliongoza mjadala uliopewa kichwa kisemacho “Mstakabali Mwema: Mjadala wa Kimataifa kuhusu Elimu kwa Mtoto wa Kike,” ulioandaliwa na mradi wa jarida maarufu la Glamour wa kuwasaidia wasichana na kuwashirikisha wasichana kutoka nchi mbalimbali duniani. Akishiriki kutokea Washington DC, Mama Obama aliungana na mwigizaji na mwanaharakati Yara Shahidi pamoja na Mhariri Mkuu wa jarida la Glamour Cindi Leive. Kwa kupitia Mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao (video-chat)wasichana kutoka Tanzania, Jordan, Peru, Uingereza na Marekani walijadili changamoto zinazowakabili na namna ya kuzikabili ili waweze kupata elimu bora. Wasanii mashuhuri kutoka katika nchi hizo walishiriki katika majadiliano hayo, ambapo nchini Tanzania mwimbaji mahiri Vanessa Mdee aliongoza kipindi cha maswali na majibu kati ya wasichana wa Tanzania na wale wa nchi nyingine.

“Wasichana wa Tanzania wanastahili kupata kila fursa ili waweze kufikia upeo wa uwezo wao,” alisema Mdee. “Nina hamasa kubwa mno ya kusaidia elimu yao na ninashukuru kuwa sehemu ya tukio hili la kuonyesha nini Tanzania na nchi nyingine zinaweza kufanya katika kuwaandaa wasichana kufanikiwa shuleni na hata baada ya kuwa wamemaliza masomo yao.”

Tanzania ni moja kati ya nchi mbili za kipaumbele katika mpango ujulikanao kama “Let Girls Learn uliozinduliwa na Rais Barack Obama na Mama Michelle Obama hapo mwaka 2015 kwa lengo la kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakwamisha wasichana kupata elimu bora itakayowawezesha kufikia upeo wa uwezo wao.

Akiwakaribisha washiriki wa Kitanzania katika majadiliano hayo Mkurugenzi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa Sharon Cromer alisisitizia umuhimu wa kuhakikisha kuwa kila msichana wa Kitanzania anapata elimu bora.

“Wanawake na vijana ndio kitovu cha jitihada zetu za kuisaidia Tanzania kuwa imara zaidi, yenye ustawi zaidi na iliyo jumuishi zaidi,” alisema Cromer. “Ni lazima tufungue fursa na uwezo wa wasichana kama hawa waliopo hapa leo iwapo kweli tunataka kuinua hali ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania na kuinua fursa kwa Watanzania wote.”