Flag

An official website of the United States government

U.S. Government Launches $30.5 Million Conservation Project to Support Conservation of Wildlife Movement Corri
4 MINUTE READ
Novemba 1, 2021

Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ilizindua mradi wa uhifadhi wa miaka mitano utakaogharimu dola za Marekani milioni 30.5 ili kukabiliana na mienendo inayotishia harakati za wanyamapori na uhifadhi wa muda mrefu wa bayoanuai nchini Tanzania. Mradi huu ujulikanao kwa jina la USAID Tuhifadhi Maliasili unatekelezwa na Research Triangle Institute International, taasisi ya utafiti wa maendeleo ya kimataifa.

Katika miongo michache iliyopita, Tanzania imepoteza angalau theluthi moja ya mifumo ya ikolojia yake na kushuhudia idadi ya viumbe vilivyo hatarini kuongezeka mara tatu. Zaidi ya hayo, takriban 25% ya mapato ya nje ya nchi yanatokana moja kwa moja na utalii—ambao kwa sehemu kubwa hutegemea sekta ya uhifadhi wa wanyamapori. Kwa kiwango cha sasa cha kupungua kwa spishi, athari kwenye uthabiti wa kiuchumi inatarajiwa kuwa kubwa.

Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, USAID Tuhifadhi Maliasili itashirikiana na Serikali ya Tanzania, jamii za wenyeji na sekta binafsi kutatua changamoto hizo. Tuhifadhi Maliasili inanuia kuunda mazingira ambamo njia za harakati zitaboresha ubora wa maisha kwa sio tu wanyamapori bali pia jamii zinazowazunguka.

Ili kutimiza malengo yake, mradi utaimarisha uwezo wa taasisi kwa wadau wa sekta ya umma na binafsi. Kupitia kuongezeka kwa ushirikishwaji wa sekta binafsi, mradi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tuhifadhi Maliasili utaimarisha sera ya udhibiti na mazingira rafiki kwenye usimamizi wa maliasili.

“Kwa kasi ya sasa ya upungufu wa viumbe, Tanzania iko njiani kupoteza kiasi kikubwa cha utalii, ambacho kitakuwa na athari kubwa za kiuchumi,” alisema Kate Somvongsiri, Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa. “Ingawa hatuwezi kubadilisha uharibifu wa awali wa wanyamapori na maliasili, kuendelea, mradi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa wa Tuhifadhi Maliasili utawezesha usimamizi endelevu katika ngazi ya jamii na kitaifa.”

Katika kuongeza matokeo chanya, Tuhifadhi Maliasili itashirikisha na kuwawezesha wanawake na vijana kwenye ngazi za mitaa na kitaifa, kuwahimiza kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi, kuchukua majukumu ya uongozi na kuwajibika kwenye maliasili zinazowazunguka.

Akizungumza katika hafla hii, Bi Somvongsiri alisema, “kutumia mtazamo wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi wa mwaka 2021, napenda kuchukua fursa hii kuwatangazia kwamba ulimwengu unakabiliwa na shida kubwa ya hali ya hewa. Mabadiliko ya hali ya hewa sio tuu tishio lililopo, bali ni janga linalotishia kasi ya maendeleo, pia yanazidisha ukosefu wa usawa duniani; kuongezeka kwa uhaba wa maji na chakula, hitaji la misaada ya binadamu na ongezeko la wakimbizi; na kuchangia migogoro. Miradi kama Tuhifadhi Maliasili ni muhimu katika kuzuia hali mbaya zaidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.