Serikali Ya Marekani Yafadhili Warsha Na Tamasha La Siku Nne Kwa Wanamichezo Wenye Ulemavu

Deputy Chief of Mission Virginia M. Blaser shows off her juggling skills with a group of athletes with disabilities at the inauguration of a sports for disability workshop organized by the University of Kentucky and the Tanzanian Paralympic Committee.
Serikali Ya Marekani Yafadhili Warsha Na Tamasha La Siku Nne Kwa Wanamichezo Wenye Ulemavu
Serikali Ya Marekani Yafadhili Warsha Na Tamasha La Siku Nne Kwa Wanamichezo Wenye Ulemavu

Dar es Salaam, TANZANIA.  Chuo Kikuu cha Kentucky nchini Marekani na Kamati ya Michezo ya Walemavu Tanzania (Paralympic) wamezindua warsha na tamasha la siku nne kwa ajili ya wanamichezo walemavu kutoka Tanzania na Kenya katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Warsha hii inayofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inajumuisha wakufunzi na makocha kutoka Marekani, Uingereza na Kanada ambao wanatoa mafunzo ya riadha, kunyanyua vitu vizito, volleyball na mpira wa miguu. Tamasha hili ni awamu ya kwanza ya programu ya mabadilishano ambapo makocha na wasimamizi wa michezo wapatao 17 kutoka Tanzania na Kenya watakwenda nchini Marekani kushirikiana na wenzao kutoka katika majimbo ya Kentucky na Indiana.

Balozi Mdogo wa Marekani nchini Tanzania Bi. Virginia M. Blaser alisema “Tayari Serikali ya Marekani ina uhusiano imara na Kamati ya Paralympic ya Tanzania na ina historia ya kuwa na programu za mabadilishano kama hii. Kwa kufanya kazi pamoja tunaweza kujenga jamii bora ambamo raia wetu wote bila kujali iwapo wana ulemavu ama la, wanaweza kushiriki katika michezo na ambamo sote tunaweza kunufaika kutokana na ushiriki huo katika nchi zetu.”

Kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam.