Toleo Jipya: Machi 3, 2020
Raia wote wa kigeni ambao si wakazi halali wa kudumu wa Marekani na ambao walikuwa katika Jamhuri ya Watu wa China, isipokuwa katika mamlaka maalumu zinazojitegemea za Hong Kong and Macau, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au katika nchi zote za ukanda wa Schengen katika kipindi cha siku 14 kabla ya kuwasili kwao nchini Marekani, wamezuiwa kuingia nchini Marekani, kwa mujibu wa Tamko la Rais. Iwapo unaishi, umetembelea hivi karibuni au unatarajia kutembelea au kupitia China, Iran au nchi yoyote ya ulaya ya ukanda wa Schengen (ambazo ni Austria, Ubelgiji, Jamhuri ya Czech, Denmark, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Hungary, Iceland, Italy, Latvia, Liechtenstein, Lithuania, Luxembourg, Malta, Uholanzi, Norway, Poland, Ureno, Slovakia, Slovenia, Hispania, Sweden, na Uswisi) kabla ya kupanga safari ya kwenda Marekani, unashauriwa kuahirisha miadi yako ya mahojiano kwa ajili ya kupata Viza hadi itakapofika siku 14 kabla ya tarehe ya kuondoka katika nchi hizo.