Uzinduzi Rasmi wa Ushirikiano Baina ya Mradi wa Kizazi Kipya Unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani na Benki ya Barclays

Dar es Salaam: Oktoba 11, 2019, Mradi wa Kizazi Kipya unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani ulizindua ┬árasmi ushirikiano na Benki ya Barclays kuboresha na kuongeza fursa kwa vijana kuendeleza ajira kupitia mafunzo ya ufundi. Benki ya Barclays imechangia fedha za Kitanzania 10,764,000/= kwa Mradi wa Kizazi Kipya, kusaidia wasichana sita zaidi wanaoshiriki. Washiriki sita wapya – wanne kutoka Dar es Salaam na wawili kutoka Dodoma – watafanya mafunzo ya ufundi katika taasisi zinazosimamiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Fedha zilizotolewa zitagharamia ada ya masomo ya wanafunzi na vifaa vya kuanzia biashara.

Serikali ya Marekani, kupitia programu za maendeleo kama mradi wa USAID wa Kizazi Kipya, inakusudia kupunguza maambukizi na athari za VVU kwa kuwawezesha wazazi, watoto walio katika mazingira hatarishi na vijana kupata mahitaji yao wenyewe. Hii ni pamoja na kubadilisha maisha ya vijana walio katika mazingira hatarishi kwa kuwapa masomo ya ufundi na vifaa vya kuanzia biashara.

Mwaka uliopita, mradi wa Kizazi Kipya ulitoa ufadhili unaohusiana na vijana takribani 3,500 kuhudhuria mafunzo ya ufundi, ikijumuisha vijana karibu 70 ambao walikuwa wakiishi na / au wanafanya kazi mitaani. Ustadi huu unawawezesha kujikinga vyema kutoka kwenye hatari tofauti, pamoja na zile zinazoweza kusababisha hatari ya VVU au unyanyasaji wa kijinsia.

Serikali ya Marekani inajivunia kuwa mshirika wa Tanzania yenye wananchi wenye afya bora, pamoja na juhudi za kufanikisha udhibiti wa janga la VVU / UKIMWI.