Flag

An official website of the United States government

Uzinduzi wa AWE Mkoani Kagera
2 MINUTE READ
Mei 2, 2023

Tarehe 2 Mei, Ubalozi wa Marekani ulizindua Mafunzo kwa Wajasiriamali Wanawake (AWE) mkoani Kagera. AWE ni Programu inayoongozwa na Ikulu ya Marekani ikilenga kuinua maendeleo na ustawi wa wanawake kwa kuwasaidia wanawake wajasiriamali duniani kote. Wanawake 35 wa Kitanzania watashiriki katika mafunzo ya wiki 13 yatakayotolewa kwa njia ya mtandao na kuendeshwa na SELFINA taasisi mbia wa programu ya mabadilishano inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani na kufanyika katika Hoteli ya BCD Stella, Bukoba.

Programu ya AWE mkoani Kagera ni programu ya tisa ya mpango huo kuendeshwa nchini Tanzania ikiwa ni ya pili inayojumuisha mafunzo ya Kiingereza. Mikoa mingine iliyofaidika na mafunzo hayo ni Dar es Salaam, Iringa, Zanzibar, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Pwani (Bagamoyo) na Kigoma. Kupitia programu hii washiriki watajifunza jinsi ya kuandaa mipango ya biashara, kuandaa matangazo ya biashara zao, kuimarisha stadi za kujenga mitandao na kujenga uwezo wa kuongoza na kusimamia biashara zao na hivyo kufanikiwa kama wamiliki wa biashara hizo. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Yohana Sina, Bw. Famba Kazimoto aliyemuwakilisha mwanzilishi wa Omuka Hub, Mhe Neema Lugangira na Afisa wa Ubalozi wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Utamaduni Chad Morris.