Vitu Vinavyoruhusiwa na Visivyoruhusiwa Ubalozi wa Marekani

Wageni wanaohitaji huduma za konsula hawaruhusiwi kuingia na vitu vyao binafsi vifuatavyo ndani ya ubalozi.

**TAARIFA MUHIMU—Kuanzia 15 Mei, 2018, Ubalozi hautahifadhi mali zozote binafsi za wageni wanaohitaji huduma za konsula.  Wageni wanatakiwa kuacha vitu visivyoruhusiwa na ubalozi nyumbani au kutafuta utaratibu mwingine mbadala wa jinsi ya kuhifadhi vitu hivyo.

Vifaa/vitu vifuatavyo haviruhusiwi na havitahifadhiwa na wafanyakazi wa Ubalozi:

 • Simu za mkononi, kompyuta na vifaa vingine vya umeme pamoja na vipimo vya mazoezi
 • Vifaa vya muziki kama CD’s, diski mweko, vipaza sauti
 • Kamera au vifaa vya video
 • Tochi
 • Viberiti na aina zake
 • Silaha au kitu chochote kitakachoweza kutumika kama silaha
 • Visu na vitu vyenye ncha kali
 • Mikoba na mifuko yenye ukubwa Zaidi ya 10” x 10” (25cm x 25cm)
 • Vioevu, vimininika, erosoli, mafuta na aina zote za unga (isipokuwa hizi chini)

Vifaa vifuatavyo vinaruhusiwa:

 • Kiwango kidogo cha vipodozi
 • Kiwango kidogo cha chakula cha mtoto, maziwa
 • Kiwango kidogo cha nepi za mtoto
 • Mikanda ya nguo
 • Saa za mkononi zisizo na teknolojia ya Bluetooth
 • Funguo
 • Dawa zisizo katika hali ya kimininika
 • Vigari ya kubebea watoto ambavyo vinatosha kupita kwenye mashine ya x-ray

**Toa taarifa kama una kifaa tiba mwilini mwako kabla ya kukaguliwa**