Flag

An official website of the United States government

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mkurugenzi Mkazi wa USAID/Tanzania Wakabidhi Ruzuku
Kwa Mashirika ya Vijana Zanzibar
15 MINUTE READ
Novemba 30, 2021

Zanzibar Novemba 30, 2021 – Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID/Tanzania) Bi. V. Kate Somvongsiri wamekabidhi msaada wa Dola za Marekani milioni 1,052,564.82  kutoka  Serikali ya Marekani kwa mashirika 16 ya vijana kwenye hafla ya USAID Inua Vijana (Feed the Future Advancing Youth) katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

Mradi huu wa USAID Inua Vijana unaotekelezwa kwenye mikoa ya Iringa, Mbeya, na Zanzibar, unasaidia vijana wa vijijini, wenye umri wa miaka 15-35, kujihusisha na biashara ya kilimo na minyororo mingine ya thamani vijijini na kuongeza fursa zao za kiuchumi huku wakikuza uongozi na maisha bora.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bi. V. Kate Somvongsiri, alibainisha kuwa “Serikali ya Marekani imejitolea kusaidia vijana wa Tanzania, pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania kufikia Dira ya 2020 na Dira ya 2025, ambayo inalenga kuinua maisha ya Watanzania.”

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mkurugenzi Mkazi wa USAID walikutana na vijana 45 walio nufaika ambao walionyesha  jinsi wanavyo sindika bidhaa zao zikiwemo mtindi,

jamu za matunda, asali, vyakula na unga wa moringa.

Maelezo Kuhusu Wafadhiliwa:

  1. Cube Zanzibar: Cube Zanzibar hutoa huduma za mafunzo ya awali ya biashara ya kiatamizi na msaada ya kifedha na uharakishaji wa biashara kwa wanzishaji na wafanyabiashara ndogondogo Zanzibar. Lengo lao ni kuhakikisha mawazo ya biashara yanatimia na biashara zinaboreshwa. Shirika hili linafanya kazi katika nafasi ya sekta binafsi inayokua Zanzibar na chaguo la muundo wake na utoaji huduma linatokana na imani yao kwamba umakini wa utekelezaji unahitajika ili kuruhusu mawazo ya biashara, wajasiriamali watarajiwa na biashara mpya zinazoanzishwa kustawi. Kusudi lake ni kuchochea uvumbuzi na ubunifu, kwani inaamini kuwa hizo ni sifa muhimu za jamii yenye mafanikio ambayo itaweza kudumisha ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu.
  1. Aatif Aquaponics Limited: Aatif Aquaponics Limited ni kampuni ya kilimo bora cha tija iliyosajiliwa Zanzibar mnamo June 2018. Kampuni hii inazalisha bidhaa za vyakula vya afya zenye thamani ya kilimo iliongezwa kwa kutumia mbinu za kilimo bora. Pia inakuza uelewa na inakuza utumiaji wa kilimo bora kisiwani Zanzibar. Aatif Aquaponics Limited ina utalaamu na washauri katika kilimo cha hydroponics (kilimo ambacho hakitumii udongo katika upandaji wa mazao), kilimo / bustani samaki, kilimo cha uyoga mahiri, uzalishaji wa makaa ya nazi mbadala, kilimo cha mwani, utengenezaji wa bidhaa ya mwani uliongezwa thamani, kilimo cha matango bahari, usimamizi wa hasara baada ya kuvuna na matumizi ya chumba maalum cha baridi kwa ajili ya kuhifadhi mazao, teknolojia, habari na mawasiliano katika kilimo biashara, ukuzaji ujuzi, ujasiriamali wa kilimo, uhusiano wa masoko, na programu za ujasiriamali tayari kwa wawekezaji wa kilimo.
  1. Uwezeshaji Wa Jamii Zilizotengwa (E-MAC Tanzania): E-MAC Tanzania ni Shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa na kufanya kazi Tanzania bara na Zanzibar. E-MAC inatazama jamii ilioyowezeshwa na ustawi endelevu. Dhamira yake ni kuwezesha jamii zilizotengwa, pamoja na vijana, kustawi kwa kukuza mipango endelevu na kuungana na washirika wengine wenye nia moja.
  1. The Pemba Island Relief Organization (PIRO): PIRO ilisajiliwa mwaka 1997 ili kuboresha maisha na ustawi wa watu wa Zanzibar kwa kuungana na kuongeza juhudi za serikali katika kuleta maendeleo. Lengo kuu la asasi hiyo nikuchangia katika upatikanaji kwa haki za vijana za kujiendeleza Zanzibar kupitia uwezeshaji, ulinzi na uimarishaji wa maisha bora. PIRO inatazama haki sawa ya kiuchumi na kijamii Zanzibar kwa wote. Dhamira yake ni kutetea na kuunga mkono juhudi za kijamii wa kina kwa njia ya utawala bora unaowajibika. Utaalamu na kujitolea kwa PIRO kunalenga katika kusaidia jamii, vikundi, na watu binafsi ili kukuza, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi ambayo husababisha raia wake kuwa wenye afya, ufahamu, kujitosheleza na kuwajibika. PIRO inasaidia pia shughuli za ulinzi wa kijamii ambazo hutoa ushirikishwaji na kujenga uwezo, kupitia kujenga ujuzi, ushauri wa kibiashara na usaidizi kwa wanawake na vijana wa kiume wanaoingia kwenye soko la biashara.(Kumbuka: Shirika hili linapokea ruzuku mbili tofauti.)
  1. Zanzibar National Chamber of Commerce (ZNCC): ZNCC ni muungano mwamvuli wa sekta binafsi Zanzibar, ambao kazi yake kuu ni kutetea na kushawishi kwa niaba ya wanachama wake katika majukwaa mbalimbali makubwa na madogo ya kitaifa. Kazi ya ZNCC nikukuza ukuaji wa biashara Zanzibar kwa kueleza mapendekezo yalioandaliwa vyema ili kuondoa vikwazo vinavyo wakabili wafanyabiashara; kukuza umoja wa wadau ndani ya sekta binafsi; kuwezesha biashara za Zanzibar, hasa zinazoanzishwa kupata ujuzi, masoko, ubia, fursa za uwekezaji, na rasilimali fedha; na kushirikiana kwa karibu na serikali ili kuifanya Zanzibar kuvutia wawekezaji. ZNCC inashirikiana na wadau mbalimbali wenye dira inayofanana kushughulikia vikwazo vya kufanya biashara. Kwa mfano, BEST Dialogue, Trademark East Africa, Mradi wa ENGINE wa USAID, na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) walikuwa na wamekuwa washiriki wa muda mrefu wa ZNCC.
  1. Zanzibar Youth Care Organization (ZYCO): ZYCO, ilisajiliwa Februari 2018, na shughuli zake zinalenga kuwajengea uwezo vijana wa kike na wa kiume Zanzibar kuwa wastahimilivu, wenye uwezo na maarifa ili kukabiliana na changamoto za kijamii na ushirikishwaji katika nyanja zote za maisha. ZYCO ilianzishwa na wanufaika na wahitimu wa mradi wa FTFT-AY. Lengo kuu la shirika ni kuchangia katika utambuzi wa uongozi wa vijana na ustawi wa kiuchumi.
  1. IMED Foundations: Msingi wa Ujasiriamali, Usimamizi, na Maendeleo (IMED) ni shirika lisilo ya faida linalobobea katika kujenga watu binafsi, mashirika na jamii ili kutambua uwezo wao kamili, hasa katika stadi za maisha, ujasiriamali, uwezo wa kuajiriwa kwa vijana na uwezeshaji kwa wanawake kiuchumi. Taasisi hii inafanya kazi Tanzania nzima ikifanya kazi kwa karibu na washirika kutoka sekta ya umma na binafsi. Maeneo makuu ya msingi ya IMED Foundation ni ukuzaji wa uwezo kupitia mafunzo, kambi za mafunzo, uvumbuzi na changamoto za kuanza, kufundisha, mafunzo, mafunzo ya awali  ya biashara, na utetezi wa sera jumuishi. IMED Foundation hapo awali ilifadhiliwa na wafadhili mbalimbali kama Mott Foundation, Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Denmark, Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Norway na miradi mingine ya USAID.
  1. The Launchpad Limited: Launchpad ni shirika lisilo la faida la maendeleo ya mtaji wa binadamu ambayo kwa zaidi ya miaka mitatu inaendelea na operation zake. Dira na dhamira ya Launchpad imejikita katika ukuzaji wa ujuzi na stadi za maisha, na mafunzo ya ushirikishwaji sawa, ambapo, mkazo ni makundi yaliyotengwa katika jamii  (vijana, wanawake na watu wanaoishi na ulemavu). Shirika hili limeboboea katika kutoa mafunzo ya ustadi wa karne ya 21 kwa ajili ya kusaidia vijana kupata elimu na kuwatayarisha kwa ajira na ujasiriamali/kujiajiri, kufundisha na kuwashauri vijana kusaidia njia za ajira, kupitia mafunzo ya kazi na kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo na za kati. Launchpad pia inafanya kazi na mashirika binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mengine kusaidia biashara zinazoongozwa na vijana kupitia mafunzo ya ujasiriamali, na kuajiriwa.
  1. University of Iringa, Centre for Entrepreneurship, and Innovation (CEI) and its Kiota Innovation Hub: Chuo Kikuu cha Iringa, kupitia CEI na Kiota Hub, kimekuwa kikiongoza juhudi za kukuza ujasiriamali na uvumbuzi katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Ili kuwahudumia vyema vijana wake ndani na nje ya Chuo Kikuu, CEI ilianzisha Kitovu cha Ubunifu cha Kiota, ambacho ni nafasi wazi kukuza mawazo, mabadiliko ya mawazo, mitandao na uundaji ushirikiano kwa ajili ya uwezeshaji wa jamii. Kiota Hub ilichochea uundaji wa waanzishaji biashara ndogo ndogo 160 na waanzishaji wa hizo biashara ndogondogo zingine 40 mpya ambazo kwa sasa wanashauriwa. Hub imefanikiwa kuwafikia zaidi ya vijana 1,000 kupitia matukio na warsha zaidi ya 50 ikiwemo “Maisha Baada ya Chuo Kikuu,” hackathons “ Iringa Sparks,” Hafla za kuhamasisha, na tukio la kila mwaka linaloitwa “Anzisha Biashara Yako”. Mwaka 2019, Kiota Hub ilishirikiana na Sahara Ventures katika juhudi ya kukuza biashara zinazomilikiwa na wanawake kupitia Mradi wa Kushawishi Wasichana 100. Kama matokeo ya mradi huu, wasichana wote 100 walifanikiwa kuanzisha na kuendesha biashara zao wenyewe.
  1. CV People Tanzania: CV People Tanzania hutoa huduma za kuajiri na kukuza vipaji maalum. Kampuni ina mitandao iliyopo na inayoendelea kote Tanzania bara na Africa na inawaunganisha wanaotafuta kazi na waajili na ajira zinazopatikana nchini Tanzania, Zimbabwe, Zambia, Uganda na Afrika Kusini, ikiwa ni waajiri zaidi ya 2000 katika mtandao wake wa Tanzania peke. Pia wanashiriki ujuzi unaohitajika na waajiri katika nchi zilizotajwa na vyuo vikuu ili wakufunzi na waelimishaji waweze kuwatayarisha vyema vijana kwa soko na kuboresha mitaala na moduli za mafunzo. CV People Tanzania ni mwanachama wa mashirika kama vile Chama cha Waajiri Tanzania, Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, na Mtandao wa Wanawake katika Usimamizi Nchini Tanzania. Kwa kutambua kazi yake, CV People Tanzania hivi karibuni ilipokea tuzo tatu kutoka kwenye nembo ya Mwajili bora Afrika, Ubora wa Kimataifa wa Rasilimali Watu, na kuwa mshindi wa pili katika kundi la Ubora wa Biashara Afrika Mashariki katika sekta ya huduma. CV People Tanzania ilichaguliwa kuwa miongoni mwa Biashara 100 Bora zinazoongozwa na Wanawake Afrika Mashariki na Invest2 Impact.
  1. Pamoja Youth Initiative (PYI): PYI ni asasi isiyo ya kiserikali na isiyo ya faida inayoongozwa na vijana wenye makao yake makuu Zanzibar iliosajiliwa rasmi 2015. PYI ilianzishwa kwa dhamira ya kuimarisha ushilikishwaji na ushiriki wa vijana wa Kizanzibari katika kuleta mabadiliko chanya ya kijamii sambamba na kutambua uwezo wao na kuchangia maendeleo ya jamii. Chini ya mpango mkakati wake wa 2018-2023, PYI inaangazia maendeleo ya uongozi wa vijana, riziki na ushirikishwaji wa kirai wa vijana, na demokrasia. Chini ya kipengele cha ukuzaji wa uongozi wa vijana, PYI inabuni na kuwezesha programu za mafunzo ya uongozi na ushauri ili kuongeza na kasi ya ushiriki wa vijana katika nafasi za kufanya maamuzi. PYI iliendesha mafunzo kadhaa juu ya ukuzaji wa uongozi, kupitia mipango kama vile, Mradi wa Mafanikio wa Vijana Zanzibar, Mafunzo ya Uongozi na Chapa, na Mpango wa Ushauri wa Wanafunzi wa Sekondari Zanzibar. Pia kupitia washirika wake PYI ilisaidia vijana 9 kuhudhuria programu tofauti za uongozi za kimataifa ambazo ziliwapa uwezo wa kuchukua majukumu ya uongozi katika maisha yao ya binafsi na kubadilisha mashirika yao.
  1. Seedspace: Kampuni ya Seedspace, ilisajiliwa nchini Tanzania mwaka 2018, ni kundi la kimataifa lenye dhamira ya kusaidia maisha ya watu kupitia teknolojia na ujasiriamali katika masoko yanayoibukia. Dhamira ya Speedspace inafanikiwa kwa kufanya programu, matukio, na miradi tofauti katika sekta ya kilimo, afya, elimu, nishati safi na ujumuishaji wa kifedha. Speedspace inaunganisha wadau ndani ya mifumo ikolojia, huunda makampuni kwanzia mwanzo na kuwekeza katika makampuni ya ukuaji wa juu kupitia mipango mbalimbali; ikijumuisha upelelezi wa kuanzia, ujenzi wa kampuni, vibanda vya kufanya kazi pamoja, na programu za kuongeza kasi. Speedspace ina mtandao wa maelfu wa wajasiliamali, wawekezaji, vikundi vya mafunzo maalum ya awali, mashirika, na mashirika ya serikali kutoka nchi zaidi ya 80. Tangu kuanzishwa kwake, Speedspace imekuwa ikifanya kazi na wajasiliamali  tofauti katika sekta tofauti ili kuongeza thamani zao na kuwafanya kuwa tayari kwa masoko makubwa. Hivi majuzi Speedspace ilifanyakazi na waanzishaji sita kupitia mpango wao wa kuongeza kasi na kuwafunza na kuwekeza hadi dola za Marekani 250,000 katika biashara zao. Biashara hizo zilijumuisha: Yamee Afrika ambaye anaufanya mfumo ikolojia wa teknolojia ya biashara ya simu kwa kujumuisha zaidi na kufikiwa barani Afrika; Kilimo Fresh, Biashara ya Mtandao (E-Commerce) jukwaa la usambazaji wa mazao linalounganisha wakulima wadogo na wanunuzi wa mazao nchini Tanzania kwenye soko la haki na uhakika; na Agripoa, kilimo kinachozingatia hali ya hewa na mfumo wa usimamizi wa shamba uanoendeshwa na data unaomsaidia mkulima kusimamia shamba lake kwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati ufaao.
  1. Zanzibar Fighting Against Youth Challenges Organization (ZAFAYCO): ZAFAYCO inatarajia kuona vijana wa Kizanzibari kuwa na uwezo wa kushughulikia changamoto za sasa za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ili kufikia hili, ZAFAYCO inafanya kazi katika maeneo matatu muhimu: Ushirikishwaji wa vijana wa kiraia, uwezeshaji wa kiuchumi, na afya. Katika ushirika wa raia, shirika linalenga katika kuongeza ushiriki wa vijana katika vyombo vya kufanya maamuzi na kuimarisha ujuzi wa uongozi, utetezi, ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu, na mipango ya kujenga amani; na kuongeza ushiriki wa wapiga kura katika vipindi mbalimbali vya chaguzi za Zanzibar. Shirika lina uzoefu mkubwa na utalaamu wa utekelezaji wa mipango ambayo inashughulikia ushiriki duni wa vijana katika vyombo vya kufanya maamuzi. Kwa mfano Pemba walitelekeza mradi wa programu mbalimbali zenye matokeo ya muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo vijana 315 viongozi wa serikali za mitaa kuweka kikosi kazi cha pamoja ili kuongeza ushiriki wa vijana na kusukuma ajenda ya vijana katika ngazi ya serikali za mitaa. Asasi iliandaa mipango na midahalo mbalimbali ya kuongeza ushiriki wa vijana na kuchangiza ajenda ya maendeleo ya Taifa ikiwa na pamoja na sera ya maendeleo ya vijana Zanzibar, marekebisho ya mpango kazi wa ajira kwa vijana wa Zanzibar, na ilani ya vijana Tanzania ya mwaka 2015 hadi 2020. ZAFAYCO pia ilifanya tathimini mbalimbali zilizoonyesha haja ya ushirikishwaji wa vijana katika mchakato wa maendeleo, ikiwa ni pamoja na mfumo wa ikolojia wa vijana wa Zanzibar, uliofadhiliwa na Benki ya Dunia mwaka 2017; ramani ya jumuiya ya kiraia ya vijana Zanzibar mwaka 2018, iliofadhiliwa na Umoja wa Ulaya; na kuendeleza hifadhi data za vijana wa Zanzibar na tathimini ya mazingira kuhusu hali ya afya ya uzazi ya vijana Zanzibar mwaka 2018 hadi 2019, chini ya msaada wa Muungano wa Afya ya Uzazi wa Vijana Tanzania.
  1. Zanzibar Technology and Business Incubator (ZBTI): Zanzibar Technology and Business Incubator Limited ni shirika lisilo la faida linalopatikana Zanzibar, Tanzania. ZTBI ni shirika la kipekee linalojikita katika kukuza ubunifu na ujasiriamali miongoni mwa vijana kati ya miaka 15-35 Zanzibar. Dhamira ya ZBTI ni kuchochea uanzishaji wa biashara na ukuaji wa biashara hadi kufikia mafanikio, muundo mzuri, unaosimamiwa vyema na wenye tija kikamilifu kwa manufaa ya watu wote wa Zanzibar.